Na Victor Masangu, Zanzibar
Zaidi
ya wakulima 1200 wamejitokeza kuwekeza katika kilimo cha zao la vanilla
visiwani Zanzibar kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kuondokana na
wimbi la umasikini.
Wakulima
hao wameamua kuungana na kujikita zaidi katika kilimo hicho ambacho
wanaamini kitaweza kuleta mabadiliko chanya ya kuchochea ongezeko katika
pato la Taifa pamoja na kuleta maendeleo kwa mkulima mmoja mmoja.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Vanilla International Limited
Saimon Mkondya ambao walifanya ziara kwa ajili ya kutembelea na kunionea
mashamba hayo ya Vanilla alisema lengo kubwa ni kuwasaidia wakulima
kujikwamua kiuchumi.
"Kilimo
cha zao hili la Vanilla kinasaidia Sana wakulima na kwamba kitaweza
kuleta mabadiliko chanya zaidi ya kimaendeleo pamoja na kuchangia katika
pato la Taifa kwa hiyo ni zao muhimu sana na linatajwa kuwa zao namba
mbili kwa Bei kubwa duniani,"alisema Mkurugenzi huyo.
Aidha
mkurugenzi huyo alibainisha kuwa kwa Sasa wamefanikiwa kuwapa ajira
vijana wapatao 270 na kuwahimiza vijana wengine kushiriki kwa wingi
katika kilimo cha zao Hilo.
Kwa
upande wake kijana mmoja anaefahamika kwa Jina la Mohammed Mzee miaka
27 Mkazi wa Zanzibar ameeleza kuwa ameacha kutumia Dawa za Kulevya aina
ya Bangi mara baada ya kushiriki katika Kilimo cha Vanila ambacho
kimebadilisha Maisha yake.
Ameeleza
kwa takribani miaka 10 amekuwa akitumia bangi pamoja na kuishi maisha
ya maskani ambapo hakuwa na muelekeo katika Maisha yake.
“Kiukweli
sikuwa kwa Miaka mingi nilikuwa naishi maisha ya Maskani na kutumia
Bangi ila baada ya kushawishiwa kujiunga na Kilimo cha Vanila nimeacha
kutumia na sasa naelewa mustakabali wa Maisha yangu,” ameeleza.
Ameongeza
kwamba kilimo hicho kina mfanya anakuwa anakuwa na Shughuli nyingi na
kukosa muda wa kukaa Maskani na kutumia bangi na starehe nyingine.
Ameeleza
kwa sasa anauhakika wa kuingiza kiasi kisichopungua Laki 350 na
kuendelea baada ya kuingia katika kilimo hicho ambapo anashirikia katika
shamba la Vanila Internation Limited Zanzibar huko bungi.
No comments:
Post a Comment