Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Wakaguzi wa ndani 140 kutoka halmashauri 69 nchini( hawapo pichani), wanaoshiriki mafunzo ya siku tatu ya namna ya kukagua kwa ufanisi taarifa za fedha, yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali katika Kituo cha Mikutano cha NBAA, Bunju, Dar es Salaam.
Na Josephine Majula na Scola Malinga WFM - DSM
WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewataka
Wakaguzi wa Ndani kufanya kazi zao bila kupepesa macho kwa kufichua
upotevu wote wa fedha za umma kwa kuwa Serikali ipo na itawalinda ili
kuhakikisha fedha za umma vinatumiwa vizuri kama ilivyopangwa
Dkt.
Nchemba ametoa maelekezo hayo wakati akifungua mafunzo ya Siku tatu ya
Wakaguzi wa Ndani wapatao 140 kutoka Halmashauri 69 nchini, kuhusu
ukaguzi wa taarifa za fedha kutoka katika Taasisi za Umma yanayofanyika
katika Kituo cha NBAA, Bunju, Jijini Dar es Salaam.
“Wekeni
wazi upotevu wote wa fedha za umma katika miradi inayotekelezwa ili
hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wale wote watakaokuwa wametumia
vibaya fedha ya umma”, alisisitiza Dkt. Nchemba
Aidha,
Dkt. Nchemba aliahidi kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali
zinazowakabili ikiwemo ufinyu wa bajeti, vitendea kazi na wataalamu
mbalimbali wakiwemo wahandasi watakaoshiriki katika ukaguzi wa mali za
umma Pamoja na kukamilisha muundo mpya wa tasnia ya ukaguzi wa ndani ili
kuleta tija.
“Serikali
itazifanyia kazi haraka changamoto hizo ili zisiwe kikwazo katika
kutekeleza majukumu yenu ya msingi”, alisisitiza Dkt. Nchemba.
Alisisitiza
umuhimu wa wataalam hao kuyatumia mafunzo watakayoyapata kuboresha
mifumo ya ukaguzi wa ndani kwa sababu kada hiyo ni muhimu kuchangia
udhibiti wa matumizi ya serikali kuoitia ukaguzi wanaoufanya.
Kwa
Upande wa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw. Athumani Mbuttuka,
alitoa wito kwa maafisa masuuli kutenga fedha kwa ajili ya ukaguzi
katika miradi yote inayoibuliwa ili kupata thamani halisi ya utekelezaji
wa miradi hiyo.
“Kada
ya Wakaguzi wa ndani inakabiliwa na changamoto za kibajeti hivyo
ninakuomba mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mioango, kuwaelekeza maafisa
Masuuli, wakati wanaanda miradi, waweke fungu la ukaguzi katika miradi
hiyo, hatua hii itasaidia kupunguza ama kuondoa kabisa malalamiko ya
wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi yao” alisema Bw. Mbuttuka
Aidha,
Bw. Mbuttuka alielezea umuhimu wa wakaguzi wa ndani kujengewa uwezo na
ujuzi wa kufanya ukaguzi kwenye mifumo ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano ambayo inatumika kwa kiasi kikubwa ili kudhibiti upotevu wa
fedha za umma na kuongeza mapato ya Serikali.
“Tumeanza
kutoa mafunzo kwa wakaguzi wetu wa ndani ili kuwajengea uwezo wa
kufanya ukaguzi kupitia mifumo ambapo hadi kufikia mwaka 2026,
tunatarajia kuwa na wataalam zaidi ya 320 watakaopatiwa mafunzo hayo ili
kukabiliana na ushindani na mataifa mengine Jirani waliowekeza kwa
kiwango kikubwa katika taaluma hiyo” Alisema Bw. Mbuttuka
Kwa
upande wao, Mkaguzi Msaidizi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw. Emmanuel
Subi na mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo ambaye ni Kaimu Mkaguzi wa
Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, CPA Wamilika Mlangi,
waliishukuru Serikali kwa kuendesha mafunzo hayo yatakayo waongezea
ujuzi wa kufanya kaguzi mbalimbali kwa ufanisi Zaidi na hivyo kuleta
tija katika matumizi ya fedha za Serikali.
Washiriki
wa mafunzo hayo wamekubaliana kwenda na kauli mbiu isemayo: Tutakwenda,
Tutakagua na Tutatoa taarifa kama ilivyo, baada ya kupewa changamoto
hiyo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba
Wakaguzi
wa Ndani wapatao 520 kutoka nchi nzima wanatarajiwa kupatiwa mafunzo
hayo ya ukaguzi wa taarifa za fedha ili kujiridhisha kuhusu usahihi wake
kabla ya kuwasilishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG).
No comments:
Post a Comment