Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka wa katikati akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mwenyekiti wa UVCCM Kibaha mji Ramadhani Kazembe wa kulia na kushoto kwake ni Katibu wa UVCCM.
Na Victor Masangu, Pwani
Mbunge
wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amewaasa vijana kuhakikisha
wanatumia fursa zilizopo iliwemo kubuni miradi mbali mbali ambayo
itawasaidia kwa kiasi kikubwa katika kujikwamua kiuchumi.
Koka
ametoa kauli hiyo wakati wakati wa kufungua mkutano wa kwanza wa Baraza
la umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Kibaha mjini
(UVCCM) na kuhudhiliwa na viongozi mbali mbali wa chama.
Aidha
koka aliongeza kwamba vijana wanapaswa kubadilika na kuaangalia namna
ya kuweza kujiunga kwa pamoja katika vikundi ili waweze kuwezeshwa
kupata fursa ya mikopo ambayo inatolewa na halmashauri.
"Vijana
wa uvccm ni lazima kuanzisha na kubuni miradi mbali mbali kwa fursa ni
nyingi za kuweza kujikwamua na uchumi na mm nitakuwa na nyinyi bega kwa
bega katika kuwasaidia katika suala la maendeleo,"alisema Koka.
Pia
alisema lengo lake kubwa kuwasaidia vijana hao endapo wakijiunga katika
majukwaa na kuanzisha vikundi mbali mbali ili aweze kuvisapoti kwa
Hali na Mali.
Pia
aliwashauri viongozi kuwaunganisha vijana wa kada mbalimbali katika
kila kata ili wajiunge na UVCCM na waweze kunufaika na fursa mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kupata fursa za mikopo na ajira kwa wenye vigezo.
"Serikali
imetenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia vijana hao hivyo kuna umuhimu wa
vijana kuwaunganisha kwa pamoja na kujiunga na UVCCM ili wanufaike na
fursa zilizopo katika maeneo yao,"alisema Koka.
Kwa
Upande wake mwenyekiti wa UVCCM Kibaha mjini Ramadhan Kazembe pamoja
na mambo mengine amemuomba mbunge huyo kusaidia kukamilisha ujenzi wa
nyumba ya katibu wa ccm
Kazembe
alishidi kushirikiana bega kwa bega katika kuboresha maisha ya vijana
na kuimalisha mahuziano mazuri ambayo yatasaidia kuleta chachu ya
maendeleo.
Kadhali
aliongeza kuwa ataweka mipango madhubuti ya kusimamia shughuli mbali
mbali za kimaendeleo ikiwemo sambamba na suala la kujenga amani.
Baraza
hilo la UVCCM limehusisha uchaguzi wa kamati ya utekelezaji wajumbe
watu pamoja na katibu wa hamasa mmoja na kufanya kamati hiyo kuwa na
idadi ya wajumbe nane.
No comments:
Post a Comment