Na Mwandishi Wetu
Uongozi wa Kagera Sugar FC, umefikia makubaliano ya pande zote mbili ya Kuvunja mkataba na Kocha Francis Otieno Baraza.
Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa usiku wa kuamkia leo kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya Klabu hiyo, ambayo imeeleza kuwa.
"Uongozi wa klabu unapenda kumshukuru Kocha Fransic Kwa mchango wake mkubwa aliouonesha ndani ya klabu Kwa muda wote wa utumishi wake.
"Hadi leo tunafikia makubaliano haya ya kusitisha mkataba wake kwa maslahi mapana ya klabu yetu na pia Uongozi unamtakia Kila la heri katika majukumu yake mapya." Taarifa hiyo imeongeza kuwa.
"Kuelekea mchezo wetu wa Mzunguko wa 10 dhidi ya KMC ambao tunatarajia kucheza siku ya Jumanne Tar 01 NOV Jijini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba , kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha msaidizi Marwa Chacha.
No comments:
Post a Comment