Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Taifa Soka la Watu wenye ulemavu Tembo Worries imefuzu hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia, ni baada ya kuwachakaza Uzbekistan mabao (2-0).
Tembo Warriors, imefuzu kuingia 16 Bora ya Fainali za Dunia za Soka la Walemavu baada ya kumaliza ikiwa na pointi nne katika kundi lake ikiwa ya tatu nyuma ya Poland na Uzbekistan.
Tembo Warriors imekata tiketi hiyo baada ya kuwa moja ya timu nne zilizoshika nafasi ya tatu zikiwa na uwiano mzuri (best looser) baada ya kuifunga Uzbekistan, kutoka sare na Hispania na kufungwa na Poland.
Sasa Tembo Warriors watacheza na Japan katika hatua hiyo mchezo utakao chezwa kesho Jumatano Oktoba 5, 2022, kusaka tiketi ya robo fainali.
Akizungumza katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania hapa Istanbul, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohammed Mchengerwa amewataka vijana hao kuendelea kulishamirisha Taifa huku akizindua kampeni ya kuzifunga kila timu zinazokuja mbele yao iitwayo #LeteniMzungu.
No comments:
Post a Comment