Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezifungia kusajili klabu za Ligi Kuu ya NBC za Tanzania Prisons na Singida Big Stars kwa kosa la kusajili wachezaji wenyewe mikataba na klabu nyingine.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa klabu hizo hazitaruhusiwa kusajili kwa dirisha Moja la usajili.
"Uamuzi wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji umefanywa kwa kuzingatia kanuni ya 47(21) ya Ligi Kuu baada ya kuzikuta na kosa hilo. Adhabu hiyo ni kwa dirisha moja la usajili."
"Tanzania Prisons ilimsajili kipa Musa Mbise wa Coastal Union wakati ikifahamu kuwa bado ana mkataba klabu hiyo. Nayo Singida Big Stars ilimsainisha mkataba Kipa Metacha Mnata huku akiwa bado ana mkataba na Polisi Tanzania." Imeeleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa.
"Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inazikumbusha klabu zote nchini kuwa usajili wa wachezaji unafanywa kwa kuzingatia kanuni, na ambazo zitakiuka kanuni zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni." Imeeleza taarifa hiyo.
Metacha Mnata
No comments:
Post a Comment