HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

November 14, 2022

NHC kukutanisha wadau 1,000 kutoka ndani na nje ya nje


Meneja Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Sagini, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa Sera ya Ubia ya Shirika hilo utakaofanyika Novemba 16, mwaka huu. PICHA: MTANDAO.

 


SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), limesema kwamba takribani wadau 1,000 wanaotarajia kukutana nchini,  Novemba 16, mwaka huu, lengo kwenye uzinduzi wa Sera ya Ubia na kujadili fursa za ubia hususan ujenzi wa majengo.

Kati ya washiriki hao taasisi za kimataifa ni 10, balozi zaidi ya 20, kamati mbalimbali za bunge pamoja na taasisi za fedha na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Meneja Habari na Uhusiano wa shirika hilo, Muungano Saguya, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, akisema matokeo ya uzinduzi huo ni baada ya kutangazwa kwa Sera Ubia iliyoboreshwa.

Alisema mkutano huo ambao utafanyika jijini Dar es Salaam, mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na kwamba mwitikio mkubwa upo kutoka makampuni binafsi ya ndani na nje ya nchi.

“Washiriki katika uzinduzi huu ni taasisi za Serikali, vyama na bodi za kitaaluma, pamoja na wawekezaji binafsi wa ndani na nje ya nchi ambao tayari wamethibitisha kushiriki.

“Katika uzinduzi pia zaidi ya Balozi 20 na Taasisi za Kimataifa 10 zitashiriki, Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Wenyeviti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Mawaziri, Mhimili wa Mahakama na Taasisi za Fedha.

“Kutokana na hali hiyo, Shirika limeona ni vema kuchambua na kuainisha zaidi maeneo ya kutosha ya kukidhi shauku hiyo ya kujenga nchi yetu, hapo awali tulitenga maeneo 60 tu yenye viwanja au majengo yanayohitaji kuendelezwa. Kwa msukumo uliopo sasa, tumeamua kuongeza maeneo zaidi ili yaendelezwe,” alisema Saguya.

Alisema, Shirika hilo linatayarisha vitabu viwili vitakavyoelezea sera hiyo na maeneo ya uwekezaji ya NHC yaliyopo, ikiwamo maeneo yenye majengo chakavu.

“Kuzinduliwa kwa Sera ya Ubia kunaenda kufungua milango ya uwekezaji kwenye sekta ya nyumba na kwamba Shirika linaunga mkono, maono na maelekezo ya Rais Samia Hassan ya kuvutia wawekezaji nchini kwa kuruhusu sekta binafsi ambayo ni injini ya kuleta na kujenga uchumi wa Taifa letu,” alisema Saguya.


 

No comments:

Post a Comment

Pages