HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

November 15, 2022

KATIBU MSTAAFU KAMISHENI YA WACHEZAJI AUTAKA UJUMBE RT

Katibu mstaafu Kamisheni ya Wachezaji RT, John Jilala Mwandu (kulia) akirejesha fomu kwa Katibu Muhtasi wa RT, Rahel Swai.


Na Tullo Chambo


ALIYEWAHI kuwa Katibu wa Kamisheni ya Wachezaji Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tabu John Jilala Mwandu, amejitosa rasmi kugombea nafasi ya ujumbe Kanda ya Pwani katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika jijini Dodoma, Novemba 27 mwaka huu.
 
 
Mwandu, alirejesha rasmi fomu ya kugombea katika ofisi za RT jijini Dar es Salaam leo Novemba 15 majira ya saa 7: 15 mchana.
 
 
Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu, Jilala, alisema ametekeleza takwa la kikatiba, na kwamba wadau wa mchezo wa riadha wawe watulivu kipindi hiki kwani mambo mazuri yanakuja.
 
 
"Nimetekeleza kwanza takwa la kikatiba kuchukua na kurejesha fomu, wadau wa riadha wawe na subira hadi pale  kipyenga rasmi cha kampeni kitakapolia nitaanika sera zangu na wajumbe watapima, Ila mambo mazuri yanakuja," alisema Jilala.
 
 
Jilala anakuwa mgombea wa kwanza kurejesha fomu kugombea kuwakilisha Kanda ya Pwani, inayojumuisha mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara.
 
 
Zoezi la kurejesha fomu kwa wagombea, linatarajiwa kufikia tamati Novemba 20 mwaka huu.
Wengine waliokwisha rejesha fomu ni Kanali mstaafu Juma Ikangaa, Mohammed Kiganja na Suleiman Nyambui.
 
 
RT inatarajiwa kufanya uchaguzi huo, kuziba nafasi za Makamu wa Rais na Mjumbe Kamati ya Utendaji Kanda ya Pwani, ambazo ziko wazi baada ya waliokuwa wakizishikilia kujiuzulu kutokana na sababu mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Pages