Mbunge wa Same Mashariki, Anne kilango, akizungumza na wananchi wa jimbo lake.
Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango ameanzisha miradi ya viti vya kukodisha kwa ajiri ya biashara kwenye kata 14 katika jimbo lake la Same Mashariki ambazo kila kata
zimepatiwa viti 100.
Amesema
hatakikisha pesa hizo zitawasaidia kwenye kampeni za wenye viti wa
kitongoji na vijiji ifikapo mwaka 2024 kusiwe na changamoto yoyote ya
kipesa wakati wa kampeni.
Pia amewagiza Madiwa
kutunza mradi huo wa kukodisha viti hili huwe chachu ya maendeleo
katika serikali za mitaa lengo ni kuwanadi vingozi wao wa chama cha
mapinduzi.
Mhe Anne
kilango amesisitiza kata itakayofanya vizuri 2023 atawaongezea mradi
mwingine hili wajikite kutengeneza pesa ambazo zitawanufaisha kwenye
chaguzi ndogo ndogo na kuondoka na dhama za kuomba omba pesa za kampeni.
Aliendelea
kusema lengo la kuanzisha miradi hii pia ni moja ya kutekeleza Ilani ya
chama cha mapinduzi kukisaidia chama cha mapinduzi kushinda chaguzi
zote za serikali ya mtaa na uchaguzi mkuu ambao utafanyika August 2025.
Pia
Mhe Anne kilango ametoa shukran za dhati kwa muheshimiwa Raisi Samiha
Suhuru Hassani kwa kumpatia Fedha za kutosha kwa ajiri ya ujenzi wa
barabara zote za Same Mashariki ambazo barabara hizo sasa hivi
wameshakabidhiwa wakandarasi na zinafanyiwa kazi.
Kilango
pia ametoa wito kwa watanzania kwa ujumla kumuunga mkono muheshimiwa
Raisi Samiha Suhuru Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya kuijenga nchi
kwenye kila nyanja tofauti michezo barabara Upatikanaji wa maji safi na
salama na kujenga hospital za kisasa na kadharika picha na (Ashrack
Miraji).






No comments:
Post a Comment