Mwanasheria wa Serikali kutoka RITA, Joseph Mwakatobe, akitoa elimu kuhusu huduma ya wosia na mirathi kwa viongozi wa Kamati ya Maridhiano ya Amani na Ulinzi jijini Dar es Salaam leo Novemba 12, 2022.
Baadhi ya viongozi wa dini wakiwa katika mkutano huo.
Washiriki wakiuliza maswali.
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na Jumuiya ya Maridhiano, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akizungumza katika mkutano huo.
Na Mwandishi Wetu
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini(RITA) umewaasa viongozi wa Kamati ya Maridhiano ya Amani na Ulinzi kuandika wosia mapema ili kuepukana na migogoro ya mali katika familia zao pindi watakapoaga dunia.
Hayo
yamesemwa leo Novemba 12, 2022 na Mwanasheria wa Serikali kutoka RITA, Bw. Joseph
Mwakatobe alipokuwa akitoa elimu kuhusu huduma ya wosia na mirathi
katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Bw.
Mwakatobe amesema katika ulimwengu wa sasa suala la kuandika wosia ni
mtambuka hivyo jamii inapaswa kuzingatia hilo na kuchukua hatua mapema.
"Moja
ya madhara ya watu kutokuandika wosia ni kusababisha migogoro ya
kifamilia inayopelekea wanufaika kukosa haki zao katika kurithi mali za
marehemu" alisema Bw. Mwakatobe.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa kamati za Amani na Jumuiya ya maridhiano
Tanzania ambaye ni mgeni rasmi, Dkt. Shk. Alhad Mussa Salum ameishukuru
RITA Kwa kutoa elimu ya kina kwa viongozi hao na kuwaomba waendelee
kuelimisha jamii kwani huduma ya wosia ni muhimu sana katika maisha ya
watanzania.
"Napenda kuishukuru Taasisi ya RITA
Kwa elimu nzuri ya wosia lakini ombi langu ni kuendelea kutoa elimu hii
muhimu mara Kwa mara ili kila mtanzania apate maarifa haya na kuyatumia
ipasavyo" alisema Dkt. Shk. Alhad Mussa.
Hatahivyo
lengo la mkutano huu ni kufanya maridhiano ya maandalizi ya kongamano
la maadili la viongozi wa dini ngazi ya kitaifa linalotarajiwa
kufanyika Novemba 28 mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment