Serikali itaendelea kuimarisha doria za kudhibiti wanyamapori waharibifu wakiwemo tumbili na nyani wanaokula mazao na kuharibu mashamba ya wananchi.
Hayo yamesemwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Sengerema, Mhe. Tabasam Mwangao aliyetaka kujua lini Serikali itawavuna tumbili katika Kisiwa cha Juma wilayani Sengerema.
Amesema Serikali imefanya kazi ya kuyabaini na kuyadhibiti makundi ya tumbili yanayosumbua wananchi katika Kisiwa cha Juma Wilayani Sengerema.
Aidha, Naibu Waziri Masanja amesema Serikali itaendelea kuhamisha makundi hayo ya tumbili na kuyapeleka katika hifadhi nyingine zenye mahitaji ya wanyamapori .
No comments:
Post a Comment