Na Mwandishi Wetu
Ni Dakika 90 za Kihistoria kwa Mnyama Simba kualikwa kwenye Dimba la Liti mjini Singida dhidi ya Singida Big Stars.
Utakuwa mchezo wa kwanza kwa klabu hizo kukutana tangu Singida Big Stars kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Singida wanaingia kwenye mchezo huo wakitoka kutoa adhabu kali kwa Mtibwa Sugar ya mabao (5-0). Huku Singida Big Stars nao wakichagizwa na matokeo na matokeo mazuri waliyonayo mpaka sasa.
Kocha Juma Mguda amesema yuko tayari kupambana na Singida licha ya mipango yake kutibuliwa na taarifa ya Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Kuu kutoa taarifa ya kumfugia nyota na mchezaji tegemeo wa Simba Clatous Chama.
Chama Pamoja na Aziz Ki wa Yanga wamefungiwa michezo mitatu kila mmoja na faini ya laki tano kwa kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji wa timu pinzani katika mchezo uliozikutanisha klabu hizo Oktoba 23.
"Nataka niseme ukweli, sipingani na Bodi ila wanapaswa kututazama na sisi walimu tunapoumiza vichwa kuandaa mpango kazi wa mchezo husika.
"Kama walikaa kikao Novemba 4 na kufikia maamuzi ya kumfungia mchezaji wangu basi wangetoa taarifa hiyo tarehe nne na sio leo Novemba 8 siku moja kabla ya mchezo, imetuaharibia mikakati yetu yote" Mgunda ameongeza kuwa.
"Yote kwa yote vijana wako tayari kwa mchezo, wachezaji wote walioko hapa ni wa Simba na watatuwakilisha vyema kwenye mchezo huu."
Simba wanahitaji kupata matokeo chanya ili kuendelea kujiweka katika mazingira ya kukaa kileleni mwa msimamo. Singida pia wanayo nafasi ya kuwashusha Simba nafasi ya pili ikiwa watapata matokeo ya point tatu jioni ya leo.





No comments:
Post a Comment