Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini (DCEA) imeteketeza Dawa za Kulevya zenye jumla ya Kilo 1543.
Akizungumza
na wakati wa uteketezaji (uchomaji) leo jijini Dar es Salaam, Kamishna
wa Kitengo cha huduma za Sheria wa mamalaka hiyo, Veronica Matikila
kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa DCEA Gerald Kusaya k amesema zoezi
hilo la uteketezaji dawa hizo ni la kawaida na hufanyika mara baada ya
mashauri ya dawa za kulevya kuwa yamekamilika mahakamani.
Amebainisha
kuwa katika zoezi ambalo limefanyika mapema leo jumla ya kilo 569.25 ni
heroine, wakati kilo 15.3 aina ya Cocaine pamoja na tani mbili za bangi
na mirungi.
"Dawa
za Kulevya zilizotekezwa leo zimetoka katika mahakama mbalimbali
ikiwemo mahakama kuu kanda ya Dar es salaam,mahakama kuu Division ya
uhujumu uchumi,mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu, Mahakama ya hakimu mkazi
mkoa wa pwani pamoja na mahakama za wilaya" amesema Matikila.
Amesisitiza
kuwa zoezi la uteketezaji dawa za kulevya ni la kawaida, hufanyika mara
baada ya mashauri ya dawa hizo kukamilika kutoka mahakama mbalimbali
hivyo kwa mujibu wa sheria kulazimika kufanyika kwa zoezi hilo.
Ameyataja
mashauri yaliyofanikisha uchomaji wa dawa hizo yalikuwa yakisikilizwa
katika Mahakama mbalimbali ikiwemo ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es
Salaam, Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Kigamboni pamoja na Mahakama ya
Divisheni ya Rushwa.
Ameongeza
kuwa uchomaji moto dawa hizo unashirikisha taasisi tofauti mojawapo
ikiwa ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Baraza la Taifa la Madini na kwamba
uchomaji huo unafanyika kwa mara ya tatu.
Ametoa
rai kwa mamlaka husika na jamii kuendelea kutoa elimu ya madhara dawa
za kulevya ili kujenga taifa imara lenye kufuata misingi ya utu na
maadili.
No comments:
Post a Comment