Mahakama yaiamuru ilipe Sh 450m kwa wanariadha watatu
Ijumaa, Desemba 16, 2022
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha, imeamuru Kampuni ya kutoa huduma za maudhui ya vituo vya luninga - MultiChoice (T) kuwalipa Sh. 450 milioni wanariadha watatu maarufu wa Tanzania.
Imethibitika mahakamani hapo kwamba Multichoice ilitumia picha za Wanariadha Alphonce Simbu, Failuna Abdi Matanga na Gabriel Geay bila ridhaa yao wala mkataba wo wote hivyo kila mmoja imeamuriwa alipwe Sh 150 milioni..
Mbali ya adhabu hiyo, pia MultiChoice imeamuriwa iwalipe wanariadha hao asilimia 10 ya faida waliyovuna tangu kesi hiyo ilipofunguliwa hadi tarehe ya hukumu iliyotolewa Desemba 15, 2022.
Kama haitoshi, pia mahaakama imeiamrisha Kampuni ya Multichoice kuwalipa tena asilimia 10 ya faida wanayovuna kwa sasa yaani kuanzia siku au tarehe ya hukumu mpaka siku ambayo watakamilisha kulipa malipo yote.
“Mlalamikiwa (MultiChoice) katika kesi hii imethibika kwamba ni kweli alitumia picha za walalamikaji bila kupata idhini na kwa kufanya hivyo alijitengenezea faida," alisema Hakimu Mkazi Mwandamizi B. Mwakisu wa mahakama hiyo.
Wanariadha hao maarufu katika mbio mbalimbali za kimataifa walifungua kesi dhidi ya Kamouni ya MultiChoice katikati ya mwaka jana T) Limited mid wakiilalamikia kutumia picha zao kibiashara bila ridhaa yao.
Walidai mbele ya mahakama hiyo kwamba picha zao zilikuwa muhimu kwa matuumizi yao lakini kitendo cha Multichoice kuzitumia ni uporaji wenye tafsiri ya kuingilia uhuru wa mali ya mtu mali yao kitendo cha kupora haki - intellectual property rights.
Imethibitika pasi shaka kwamba picha hiizo zilitumika sehemu mbalimbali za matangazo kama vile chaneli na mabango mbalimbali za huduma ya kampuni hiyo yaliyotawanywa nchi nzima pamoja na kwenye mitandao rasmi ya kijamiii ya MultiChoice ambayo Instagram na Twitter.
Imeelezwa mahakammani hapo kwamba MultiChoice walianza kutumia picha za wanariadha hao mara baada ya kufuzu mbio za kimataifa za michuano ya Olimpiki ya Tokyo 2020 ambayo ilikuja kufanyika mwaka uliofuata yaani 2021 huko nchini Japan kutokana na tishio la ugonjwa wa Uviko 19.
Wakati wanajiandaa na michuano hiyo ndipo walipoambiwa kwamba MultiChoice wanatumia picha za wanariadha hao kibiashara wakinadi kwamba mtu anayetaka kufuatilia mashindano hayo na anunue king'amuzi cha DSTV na kulipia ili apate uhondo ya Olimpiki ya Tokyo 2020.
Katika mwenendo wa kesi hiyo, Mwanariadha, Simbu katika ushahidi wake aliieleza mahakama kwamba kitendo cha picha zake kutumika kuliimkosesha mikataba yenye malipo ya fedha nyingi kama vile kuwa Balozi wa bidhaa za Kampuni ya Habari ya Azam.
Katika utetezi wake, Wakili wa MultiChoice ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Astrid Mapunda, alipinga kuwa kampuni yao haikutumia picha hizo ili kuvuna fedha bali kuwapromoti wanariadha tajwa.
Mapunda alisema walichokifanya wao ni kuitikia wito wa Wizara yenye dhamana ya michezo iliyoagiza kuwapa sapoti wanamichezo wa Tanzania na kwamba wala sio ajabu kwani wamekuwa wakifanya hivyo mara kwa mara.
Simbu na wenzake katika shauri hilo, Waliwakilishwa na Wakili Msomi, Menrad D'Souza.
No comments:
Post a Comment