Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Lucy E Saleko akizungumza kabla ya kuanza kwa Mafunzo kwa Washeria,Waendesha mashtaka na wapelelezi walioko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini Mwanza.
Na John Bera
Wizara
ya Maliasili na Utalii kupitia Kitengo cha Huduma za Sheria imeandaa
mafunzo kwa Washeria,Waendesha mashtaka na wapelelezi walioko chini ya
Wizara hiyo pamoja na Mahakamu ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria za
kisekta na Sheria Mtambuka kwa lengo la kupunguza matukio ya ujangili wa
mazao ya misitu na wanyamapori kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.
Mwanza
na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi.
Lucy Saleko akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo jijini
amesema kuwa mafunzo hayo yameandaliwa na Kitengo cha Sheria chini ya
udhamini wa Mradi wa Kuzuia na Kupambana na ujangili wa wanyamapori na
Biashara haramu ya nyara na mazao ya misitu (CPIWT Project), UNDP na
Global Environmental Facility (GEF) chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.
“Sisi
kama kitengo cha Sheria ambao ndio waratibu wakuu wa mafunzo haya
tumekuwa tukipata changamoto hususan kwenye makosa ya ujangili na mifugo
kukamatwa kutokana na watu kuingiza hifadhini, mafunzo haya ni muhimu
pale mashauri yanapopelekwa mahakamani kuhakikisha ushahidi unatolewa
wa mtu aliyeingiza mifugo hifadhini haukwami. ‘’ Amesisitiza Lucy
Saleko.
Amesema kutokana
mafunzo hayo,Washeria,Waendesha mashtaka na wapelelezi walioko chini ya
Wizara ya Maliasili na Utalii wataongeza ujuzi katika kudhibiti
vielelezo vya ushahidi na kukusanya taarifa za ushahidi wawapo
mahakamani.
No comments:
Post a Comment