Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na timu
maalum ya kuzuia na kupambana na makosa ya mtandao limewakamata
watuhumiwa 11 wa makosa ya kimtandao.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar
es Salaam ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza na wanahabari.
Amebainisha
kuwa kukamatwa kwa wahalifu hao ni kufuatia ufuatiliaji mkali
unaoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi na Timu hiyo Maalum.
Kwamba
katika hatua hiyo Jeshi la Polisi na timu hiyo, limemkamata Alex Magoti
(26) Mkazi wa Tabora Mjini na wenzake nane kwa tuhuma za kumiliki
luninga za mtandaoni na akaunti za mitandao ya kijamii ambazo zimekuwa
zikitumika kusambaza taarifa za uongo au uzushi kuhusu, Rais Dkt Samia
Suluhu Hassan na viongozi wengine wakuu wa Serikali.
“Watuhuhumiwa
hao wamekuwa wakiweka taarifa zao za uzushi, uongo na upotoshaji kwenye
luninga za mtandaoni zinazotambulika kwa majina ya BSUN Online TV,
GATTU Online TV, TAMUTAMU online TV, KILIMANJARO online TV na
nyinginezo. Mfano wa taarifa hizo ni kama “Rais Samia akosoa vikali
utawala wa Rais JPM, aanika ukatili aliofanya (haukubaliki hata
kidogo)”,” amesema ACP Muliro.
Pia,
amesema Jeshi la Polisi limemkamata, Joseph Mzava (19) mkazi wa
Kinondoni Dar es Salaam, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo cha Biachara
Dar es Salaam (CBE), kwa tuhuma za kujinasabisha kuwa yeye ni Rais
Mstaafu Jakaya Kikwete na kufanikiwa kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu kupitia mtandao kwa kutumia laini za simu zenye usajili usio
na majina yake.
Katika
hatua nyingine Kamanda Muliro amesema wanamshikilia Li Naiyong (48)
raia wa China, ambaye anatuhumiwa kujihusisha na shughuli za kuingilia
mfumo wa mawasiliano kinyume na taratibu za nchi, na kuisababishia
Serikali hasara ya kiasi cha Shilingi Milioni Mia mbili ishirini na moja
laki moja sitini na tatu na mia sita (Tshs 221,163,600).
Kwamba
Mtuhumiwa huyo amekuwa akituma vifaa visivyo rasmi kuwaunganisha watu
kwa simu kufanya mawasiliano nje ya nchi kinyume na sheria za mmlaka ya
mawasiliano Tanzania.
Aidha,
Jeshi la Polisi linatoa rai kwa Wananchi kuwa makini na matumizi ya
mitandao ya kijamii, pamoja na kuzingatia maadili ya taaluma ya habari
na sheria zinazohusika kuepuka kuchapisha taarifa za uongo na zile
zitakazo zua taharuki kwa umma, Jeshi la Polisi halitasita kuchukua
hatua kali kwa mtu/watu wote watakao vunja sheria, kanuni na miongozo
inayoelekeza matumizi sahihi ya mitandao.
No comments:
Post a Comment