Kamishna wa Elimu Dk. Lyabwene Mtahaba, akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa elimu walio kwenye mradi wa utekelezaji wa mradi wa kuendeleza elimu nchini (TESP) unaofadhiliwa na serikali ya Canada, walipokutana kujadili maendeleo ya mradi huo.
Mwakilishi kutoka ubalozi wa Canada Rasmata Barry, akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa elimu katika utekelezaji wa mradi wa kuendeleza elimu nchini (TESP) unaofadhiliwa na serikali ya Canada, walipokutana kujadili maendeleo ya mradi huo.
Picha ya pamoja.
SERIKALI
imesisitiza kwamba kuwachapa wanafunzi sio mtazamo sahihi wa
kumfundisha bali ndio kutamdidimiza zaidi katika masomo kwa kuwa atakua
na hofu na mwalimu wa aina hiyo.
Hayo yalielezwa leo Desemba
16, 2022 na Kamishna wa Elimu Dk. Lyabwene Mtahabwa wakati wa kikao na
wadau wa elimu walio kwenye mradi wa utekelezaji wa mradi wa kuendeleza
elimu nchini (TESP)unaofadhiliwa na serikali ya Canada, walipokutana
kujadili maendeleo ya mradi huo.
Alisema kuwa watoto
wanauelewa tofauti tofauti hivyo walimu wanatakiwa kuwaelewa ,kuacha
kutumia vitisho kuacha kuwatolea maneno machafu kwani sio njia sahihi ya
kuwafundisha.
"Katika mradi huu unafundisha weledi,walimu
kuwa bora zaidi kutokana na mafunzo ya kitaaluma ikizingatiwa sasa
teknolojia iko juu hivyo basi hata ukiisha tutauendeleza kwa vitendo
Sisi wenyewe,"alisema Dk.Mtahabwa.
Aliongeza kuwa mustakabali
wa nchi unaletwa na elimu kuwa bora na ubora wa elimu ni matokeo ya
walimu kuwa bora na ndio kinachofanyika nchini .
Alisema
serikali ya Canada kupitia mradi huo imewezesha kufanyika maboresho ya
miundombinu ya baadhi ya shule,mafunzo kwa walimu sambamba na masuala ya
jenda .
Mratibu wa mradi wa TESP Cosmas Mahenge alisema
mradi huo umefadhiliwa kwa dola za Canada milioni 53 kwa kushirikiana na
serikali ya Tanzania ili kuendesha mradi huo.
Alisema fedha hizo zimesaidia katika kutoa vyakula kuoni,mafunzo kwa vitendo,kuimarisha elimu ya ualimu nchini.
"Kununulia
vifaa vya TEHAMA na kuunganisha mkongo wa taifa katika vyuo 35,ujenzi
wa chuo cha masuala ya jinsia ba ujenzi wa chuo cha elimu cha
mfano,"alisema Mahenge.
Mwakilishi kutoka ubalozi wa Canada
Rasmata Barry amesema serikali yake ipo bega kwa bega na Tanzania katika
suala zima la kuhakikisha elimu inakua bora nchini.
No comments:
Post a Comment