HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 26, 2022

YANGA SC NA 'ROHO YA PAKA' NBC PL

Na Mwandishi Wetu

Klabu ya Yanga imezidi kupepea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Soka Tanzania (NBC PL) mara baàda ya kuzichukua pointi tatu ngumu dhidi ya Azam FC, mchezo uliotoa burudani katika Dimba la Benjamin Mkapa hapo jana.



Yanga ni kama wana vinasaba na roho ya Paka kwa namna ambavyo wamekuwa wagumu kudondosha alama tatu kirahisi. Ulikuwa mchezo mgumu na wenye ufundi kwa pande zote licha ya ubora wa kikosi cha Azam katika nyakati nyingi za mchezo lakini ubora wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga uliibeba Yanga.

Ilikuwa ni burudani ya sikukuu ya Christmas yakishuhudiwa mabao matano katika derby ya Dar es Salaam, Azam ambao walikuwa wenyeji walianza kwa kujipatia bao la uongozi kupitia kwa Abdul Suleiman 'SOPU' akiitumia vema krosi ya Prince Dube.

Bao hilo ni kama liiwaibua Yanga SC kutoka mafichoni na kuanza kuupeleka moto langoni mwa matajiri wa Jiji la Dar es Salaam, Fiston Mayele akaianza sughuli kwa kutumia pasi bora ya Bernard Morisson  baada ya kumzidi ujanja Lusajo Mwaikenda.

Wakati Azam wakishangaa jinsi gani wameruhusu bao Stephen Aziz Ki akawaonyesha palipo vuj kwa shuti kali kutoka kweny usawa wa mwezi mchanga.

Mechi inayohusisha timu kubwa kufungwa mabao matano katika dakika 90 , bila shaka ilikuwa zaidi ya burudani. Nini kilitokea kiufundi?..

Timu zote mbili ziliamua kupeana nafasi na muda wa kutosha na kama hiyo haitoshi hata wachezaji ambao kwa nyakati hawana mpira walikuwa na nafasi ya kutosha sana ya kuomba huduma maeneo mengi ya uwanja ni kamaa zilikuwa mbinu za mabenchi ya ufundi ama ni wachezaji waliamua kupeana nafasi na muda.

Timu zote  zlifanana kwenye mifumo 4-2-3-1 ( Akaminko na Azizi Ki kwenye namba 10 kwenye timu zao ) na walipewa muda na nafasi ya kutosha ya kufanya wanachotaka kufanya , njia pekee ya wawili hao kupoteza mpira ilikuwa wenyewe tu waamue kupoteza lakini sio kwamba kuna presha walikuwa wanawekewa kila kitu kikawa rahisi.

Wachezaji wa pembeni wote wanne ( Kipre Jr Morisson Sopu na Moloko ) walikuwa na dhamana kubwa sana kwa timu zao kwa kufanya uwanja kuwa mpana iwezekanavyo na kuwarahisishia namba 10 wao machaguo mengi ya kupiga pasi kwa mtu ama kwenye nafasi zilizo wazi nyuma ya safu ya ulinzi ya timu zote mbili.

Idadi ya mipira waliyokuwa wanapata ni mingi sana ambayo inatosha kuletea madhara japo nyakati nyingi walishindwa kufanya hvyo, timu zote mbili bila mpira kwenye kuzuia , wanakabia juu na wachezaji wawili wawili (Mayele na Aziz - Yanga & Dube na Akaminko - Azam ) hao wawili wakianza juu nyuma yao kuna nafasi ya kutosha kwa Muguna na Sureboy kupokea mipira tena wanachukua mali na kupata muda wa kugeuka , ndio maana nafasi nyingi zilitengenezwa kwenye hii mechi kwasababu timu zote zina wachezaji wazuri sana na ukiwapa muda na nafasi kwenye mpira wanafurahia  tu uwanjani na kukupa shida.

Kipindi cha pili Azam FC ni kama walikuja juu dakika ya 46 wanaweka mzani sawa kupitia kwa yule yule toto tundu Abdul Suleiman'SOPU' ubao ukasoma (2-2) kabla ya All Ahmada kutema mpira wa adhabu uliopiwa na Aziz Ki na Farid Musa kupachika bao la tatu na la ushindi.

Viungo wa Yanga wakiongozwa na Aucho bila mpira mguuni ni tatizo, wanakosa ubora wa kunusa hatari, sio viungo halisi wa ulinzi.



No comments:

Post a Comment

Pages