Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Taasisi
ya Kimataifa ya Ithibati (Viwango) Mico imefanya Kongamano la Kwanza
lililowakutanisha wafanyabiashara jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kujadiliana na kutoa elimu na kuweka wazi masoko ya bidhaa mbalimbali ya
Biashara Halal
Akizungumza
katika kongamano hilo jijini Dar es Salaam Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania
Skeikh Hamid Jongo ameipongeza taasisi ya Halal kwa kuandaa kongamano
hilo.
Amesema kuwa uwepo wa taasisi hiyo nchini ni jambo jema kwani imekuwa ni kiu ya muda mrefu kwa wafanyabiashara na Serikali.
Skeikh
Jongo amebainisha kuwa uwepo wa taasisi hii nchini itasaidia kutoa
uthibati kwa bidhaa mbalimbali hivyo kusaidia kupenya katika masoko ya
ndani na nje na kuchangia pato la Taifa.
“Tumekuwa
tukikosa soko la kuuza bidhaa, hivyo wafanyabiashara bidhaa zao
zitathibitishwa kupitia Halal na hivyo kuongeza mapato kwa kwa
Serikali,” amesema Sheikh Jongo.
Ameongeza
kuwa taasisi hiyo itasaidia kupatikana kwa bidhaa bora kama vile za
chakula, nguo na kadhalika kwa ajili ya afya njema za wateja.
Amesisitiza
kuwa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) linaunga mkono na kupongeza
jambo hilo kwani litasaidia Mtanzania kula chakula safi, mavazi safi na
hivyo kuwa na maisha mazuri.
Pia
amesema kuwa wafanyabiashara wa Tanzania wamekuwa wakienda nchi zingine
kwa ajili ya kufata ithibati ya bidhaa zao hivyo Halal itawarahisishia
kupata ithibati ndani ya nchi.
“Kwa
kupatikana kwa Taasisi ya Halal itasaidia na kuwezesha kuwa rahisi kwa
wafanyabiashara kupata ithibati na kufanya biashara ndani na nje,”
ameongeza Sheikh Jongo.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TanTrade, Latifa Khamis amesema
soko la Halal limekwenda kimataifa hivyo kupitia Halal wafanyabiashara
watasaidiwa kujua bidhaa halali na zisizo halali ili kuweza kuhimili
soko la ndani na nje.
“Kupitia
taasisi hii wafanyabiashara hili waweze kufanya vizuri wanatakiwa kijua
Halal ni nini, naomba waitumie sana Halal kwani itawapatia ithibati ya
bidhaa zao,” amesema Latifa.
Mapema
akiongea katika kongamano hilo Naibu Mkurugenzi wa Mico Halal, Muhamed
Juma amesema kongamano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya kwanza lengo
lake ni kujadiliana, kubainisha, kuelimisha na kuweka wazi masoko.
Amefafanua
kuwa kongamano hilo limewaleta pamoja wafanyabiashara na wasio
wafanyabiashara kwa lengo la kujifunza na kupata ufahamu kuhusu Halal.
No comments:
Post a Comment