HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 30, 2023

Necta yatoa ufafanuzi matokeo ya mvulana shule ya wasichana


Na Janeth Jovin


Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limesema jinsia ya kiume inayoonekana kwenye orodha ya matokeo ya kidato cha nne katika shule ya wasichana ya Musabe ni msichana.

Kauli hiyo ya Necta inakuja ikiwa ni siku moja imepita tangu itangaze matokeo ya mitihani ya kidato cha nne uliofanyika Novemba 14 hadi Desemba 1, 2022.


Katika matokeo hayo, orodha ya majina ya wanafunzi wa shule ya Wasichana Musabe ya jijini Mwanza kuna jina la mwanafunzi wa kiume, hali iliyoibua mjadala katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari na Uhusiano wa NECTA, John Nchimbi kwa vyombo vya habari ilisema mwanafunzi mwenye namba ya usajili S5344/0125 wa Shule ya hiyo kuwa ni jinsi  ya mtahiniwa huyo ilikosewa kwa kuandikwa M (Mvulana), badala ya F(Msichana) wakati wa usajili.

Amesema Baraza litarekebisha dosari hiyo ya jinsi ili iweze kusomeka F ikimaanisha ni msichana.

No comments:

Post a Comment

Pages