HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 29, 2023

UTT AMIS YADHAMINI BONANZA LA WABUNGE

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson wameipongeza Kampuni ya UTT AMIS kwa kudhamini Bunge Bonanza 2023 lililowashirikisha Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na watumishi wa Bunge.


Walitoa pongezi hizo wakati wa hafla ya kukabidhi medali na vikombe kwa washindi wa michezo mbalimbali katika Bonanza hilo lililofana na kufanyika kwenye viwanja vya Shule ya John Merlin, Miyuji Jijini Dodoma Januari 28, 2023 ambapo ushindi wa jumla walipata wabunge.

Spika wa Bunge, Mh. Tulia Ackson pamoja na Mh. Salma Kikwete wakiongoza timu ya wabunge ya mpira wa kikapu kushangilia  ushindi dhidi ya timu ya watumishi wa Bunge.

No comments:

Post a Comment

Pages