HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 19, 2023

HATIMAYE KIMEUMANA KWA MKAPA, SIMBA YALOVYWA LOVYO

Na Mwandishi Wetu

WANASIMBA wamelia, Nchi imeshtuka lakini ndio uhalisia wa Soka hasa la kisasa lenye kuhitaji matokeo zaidi ya kuucheza mpira.

Mnyama Simba na rekodi yake ya kwa Mkapa HATOKI MTU' Jana imefika mwisho baada ya kukubali kipigo kikali kutoka kwa Raja Casablanca ya Morocco cha mabao (0-3).


Ulikuwa mchezo mgumu kwa Simba kwa kipindi cha misimu mitano sasa Mnyama kukutana nayo kwenye kiota chao ambacho kilikuwa ni kaburi la timu kubwa kufungwa hapo, lakini Raja CA wametegua mtengo.

Simba wamepoteza mchezo wa pili mtawalia ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL kundi C ambapo wiki moja iliyopita walipoteza kwa bao moja bila dhidi ya Horoya ya Guinea kabla ya hapo jana kula chuma tatu mtungi.

Mpira wa miguu ni mchezo wa maboksi yote mawili , yani nini utafanya kuzuia katika boksi lako na nini utafanya kufunga katika boksi la timu pinzani , Raja CA wameonesha nini maana yake kwa ufanisi wa hali ya juu sana.

Simba SC walikuwa wanatoka nyuma vizuri , mjongeo na watu watatu nyuma ( Inonga Sawadogo na Onyango ) Kapombe na Zimbwe pembeni zaidi ya uwanja kuwaruhusu Chama na Ntibanzokiza kuingia ndani , wanafika mpaka juu ya uwanja vizuri , shida ilikuwa maamuzi sahihi katika nyakati sahihi.

Licha ya kuutawala mchezo lakini Simba walikosa pasi ya mwisho kuwafungua Raja, mikimbio sahihi na ufanisi katika kuzimalizia wa nafasi.

Raja walikuwa wanajua kwa usahihi nini wanataka , wanazuia kwa idadi kubwa ya wachezaji kwenye umbo la mfumo wa 4-5-1 ambayo iliwapa faida katika kuzuia ndani ( vertical ) na pembeni kwa kutumia nawinga wao na wakipora mpira wapo " direct " sana kwa kutumia watatu wa mbele Khabba, Habti na Bouzok.

Dakika 90 zinatamatika Simba (0-3) na Raja inakuwa klabu ya kwanza Barani Afrika kuchukua point tatu katika Dimba la Benjamin Mkapa, ikiwa michezo tisa katika hatua hiyo Simba haijawahi kufungwa wala kupata sare, vilikuwa ni vipigo vizito na pira Biriani.


No comments:

Post a Comment

Pages