Na John Richard Marwa
Klabu ya Yanga leo inashuka Dimba la Benjamin Mkapa kuwakabili TP Mazembe mchezo wa pili wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF CC.
Yanga wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya Monastiry ya Tunisia kwa mabao (2-0).
Mchezo wa leo ni wakwanza kwa Yanga kucheza nyumbani katika hatua hiyo ya makundi huku Mazembe ukiwa mchezo wao wa kwanza kucheza ugenini wakitoka kushinda nyumbani mabao (3-1) dhidi ya Real Bamako ya Mali katika kundi D.
Ni wazi Wananchi wanahitaji ushidi Ili kujiweka sawa kusaka tiketi ya robo fainal msimu huu licha ya kuwa na kigingi katika mchezo wa leo utakao pigwa saa moja usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Yanga wanaingia kwenye mchezo wa leo wakiwa na rekodi mbaya dhidi ya wapinzani wao mara zote walizokutana hawajaahi kupata matokeo kwa Kunguru hao wa Lubumbashi.
Mazembe wamekuwa na rekodi bora dhidi ya klabu za Tanzania na wamekuwa na nyakati bora wanapokuwa katika Dimba la Benjamin Mkapa.
Swali ni je Wananchi watavunja mwiko wao wa kukosa matokeo katika Uwanja wa nyumbani katika mechi za Kimataifa.
Msimu huu Yanga wamecheza mechi tatu nyumbani kabla ya mchezo wa leo, wamecheza dhidi ya Zalan FC ya Sudan kusini na kushinda mabao (5-0). wapinzani walioonekan kuwa dhaifu zaidi.
Mchezo wa pili Yanga walicheza na Al Hilal ya Sudan na kutoka sare ya bao (1-1) kisha wakatoka suluhu dhidi ya Club Africain ya Tunisia.
Je leo Wananchi watafua dafu kwa miamba ya soka Barani Afrika Mabingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL Tupwisa Mazembe?.
Kila la heri Wananchi!
No comments:
Post a Comment