HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 19, 2023

KIPIGO CHA MNYAMA, MISS SIMBA AWATUPIA JIWE VIONGOZI....

Na John Richard Marwa

Yakiwa yamepita masaa kadhaa toka Simba SC waaangukiwe na kitu kizito hapo jana katika Dimba la Benjamin Mkapa cha mabao (0-3) dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco, mchezo wa pili hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL.

Shabiki bora, Agnes Daniel maarufu kama Miss Simba SC ametoka mafichoni na kuwakumbusha wanasimba wenzake kuwa Simba ni timu yao na hawana timu nyingine zaidi ya waliyonayo sasa hivyo lazima wakubali kuishi nayo katika nyakati zote.



Hatua hiyo imekuja kutokana na kipigo hicho cha jana pale kwenye ngome yao ya Kwa MKAPA HATOKI MTU lakini Raja walifanikiwa kutoka salama.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Miss Simba SC ameandika kwa hisia kali huku akitupa jiwe kwa viongozi na wachezaji kutimiza wajibu wao.

"Wanasimba wenzangu habari za asubuhi, najua tuna maumivu makali sana MIOYONI MWETU tunaumia na matokeo yalotokea, poleni Sana.

"Tumecheza na timu kubwa na yenye wachezaji wenye ubora wa hali ya juu, nafikiri tunajifunza kitu na Sisi ili tuwe wakubwa tuwe na wachezaji wenye ubora huo, tuvunje benki." ameandika na kuongeza kuwa.

"Tusijifiche kwenye kivuli cha Kwa Mkapa hatoki mtu wakati Sisi wenyewe ndani kwetu hapako salama.

"Kwa upande wa mashabiki sisi ndugu zangu hatuna deni, deni hili ni la viongozi na bench la ufundi na wachezaji sisi wajibu wetu tumetimiza. Niseme tu, ukitaka ubora tuvunje benki tupate wachezaji wa kaliba ya Raja." ameandika Shabiki huyo mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Klabu hiyo na mwisho ameandika.

"Poleni Sana ndugu zangu tuangalie yajayo, tusivunjike moyo tuendelee kuiunga mkono  timu iliyoko hatuna timu nyingine ndo hiyo hiyo ndo timu yetu" misssimbasportsclub


No comments:

Post a Comment

Pages