HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 26, 2023

MASHINDANO YA POLISI JAMII CUP 2023 YAZINDULIWA DODOMA

 Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amezindua mashindano ya Polisi Jamii Cup 2023 huku akisema mashindano kama hayo yanakwenda kufanyika nchi nzima.



Akizungumza kwenye uzinduzi huo mkuu wa mkoa  amewashukuru Polisi kwa kuwa na falsafa ya Polisi Jamii jambo linalofanya kuweza kujumuika pamoja kwani huko nyuma Wananchi hawakuweza kukaa pamoja na polisi ilikuwa ni Kama miujiza  kuchangamana pamoja kama marafiki.



Amesema mradi wa michezo na vijana unalengo wa kukusanya vijana na kushiriki michezo mbalimbali ili kuweza kuwa na afya Bora na kuachana na mawazo potofu ya kufanya uhalifu na badala yake kuchukia uhalifu .


"Niwatake vijana shirikianane na polisi kwa kutoa taarifa za kihalifu na wahalifu pale mnapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa Sheria," amesema


Aidha amesema  kupitia uzinduzi wa michezo hii Dodoma uhalifu utapungua au kuisha kabisa kwani Tanzania bila uhalifu inawezekana vijana mkishiriki katika mashindano haya .



Aidha alitoa rai katika mashindano yajayo kila kata iwe na timu itakayoshiriki michezo mbalimbali inayojumuisha wanawake na wanaume ili kuleta fursa sawa kijinsia.


Amesema Matarajio ya Serikali kupitia michezo hii Dodoma na Tanzania nzima kuwa salama na kwa wale vijana wasiotaka kubadilika Serikali imeweka Mipango mingi katika kuhakikisha vijana wanapata ajira ,wanajiajiri na kujifanyia shughuli mbalimbali za kupata uchumi hivyo vijana badala ya kufanya uhalifu tujishugulishe na shughuli halali kwani mikopo ya Serikali isiyo na riba ipo.


Wale vijana wachache wasio taka kubadilika kupitia Miradi ilioanzishwa na jeshi pamoja na Sera nzuri za nchi yetu wajue kuwa  jeshi la polisi lipo na sheria zitachukuliwa kwa wanaotaka kuwa mbele ya sheria.


Hivyo niwaombe wana Dodoma na watanzania kwa ujumla Kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kata hao kwani wako huko kwa ajili ya wananchi pia viongozi  wa Serikali za Mitaa na vijiji kuwapokea na kuwapa ushirikiano.


Pia amewata polisi Kata hao kufanya vikao vya usalama vya Kata na Kutoa elimu kwa Wananchi kupitia mikutano ya Mitaa Vijiji na vitongoji ili kuwaelimisha Wananchi umuhimu wa kutunza usalama ,amani kwa maeneo yao kuwepo kwenu huko iwe ni chachu ya kupunguza uhalifu.


Kwa Upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Martin Otieno amesema uzindua wa Polisi Jamii Cup umefanyika Dodoma kwa kuwa Dodoma ni makao makuu ya nchi hivyo na mikoa mingine itazindua mashindano hayo.


Amesema jeshi la polisi kupitia Miradi mbalimbali imeandaa mashindano hayo lengo likiwa ni Kutoa elimu juu ya tabia hatarishi na vijana kuwa na afya bora kupitia michezo hiyo kuwaepusha vijana kuacha tabia za uvutaji wa dawa za kulevya ,bangi na ulevi kwani nia hizo huzolotesha uchumi wa nchi.


" Kupitia Miradi tuliyoianzisha vijana wengi waendesha bodaboda na bajaji wamebadilika na tumekuwa tukishirikiana nao isipokuwa vijana wachache ambao hao wamekuwa wakiwapaka matope wenzao," amesema Kamanda Otieno.


Naye Kamishina wa Polisi jamii Faustine Shugalile lengo la mradi huo ni kuwaondoa vijana kwenye uhalifu na kuwaondoa katika Matendo hasi Kama uvutaji wa bangi, madawa ya kulevya na unywaji wa pombe ambapo kwa mradi huo kwa Dodoma unakata 208 kwa kata zote za kiaskari.


Amesema Askari watashirikiana na jamii katika kuhakikisha wanaondoa uhalifu kwa hiyari na sio kwa kukabiliana nao kwa kuwaleta vijana katika michezo na shughuli zingine.

No comments:

Post a Comment

Pages