HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 12, 2023

Mbunge Koka kutatua kero ya umeme kwa wananchi wa Kata ya Msangani

Na Victor Masangu, Kibaha

 

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka, katika kuunga juhudi za Serikali awamu ya sita ameahidi kulivalia njuga suala la huduma ya nishati ya  umeme na maji kwa wananchi wa kata ya msangani ili kuondokana na changamoto zinazowakabili.

 


Koka ameyasena hayo wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi CCM Kibaha mji ambapo amesema lengo lake kubwa ni Kuhakikisha anawatatulia wananchi wa kata ya msangani changamoto zinazowakabili katika sekta mbali mbali.

 

 Pia alisema ameweka mikakati kabambe ya kuelekeza nguvu zaidi katika maeneo yaliyopo pembezoni kwa ajili ya kufikisha huduma za kijamii.

 

 

Aidha alisema kwamba kupeleka huduma ya maji katika maeneo mbali mbali ambayo yanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji ili wananchi waondokane na adha ya huduma hiyo.

 

 

Pia alisema katika kutwkeleza ilani ya chama Cha mapinduzi atahakikisha ataendelea kushirikiana na wananchi katika kuwaletea chachu ya kimaendeleo katika sekta mbali mbali.

 

Kadhalika aliwaomba wananchi waweze kushirikiana na Serikali ili waweze kupatiwa miradi mbali mbali ya kimaendeleo kwa manufaa ya wananchi wa Jimbo la Kibaha mji na Taifa kwa ujumla.

 

Mbunge huyo hakusita kuwakumbusha viongozi kijitahidi kwa hali na mali katika kuongeza idadi ya wanachama lengo ikiwa ni katika kukiimarisha chama zaidi kiweze kushinda katika chaguzi mbali mbali.

 

Pia aliongeza ataendelea kushirikiana na viongozi wenzake wa chama wakiwemo viongozi wa matawi kwa ajili ya kukijenga chama katika ngazi mbali mbali.

 

Katika ziara hiyo Koka alitoa kadi kwa matawi yaliyopo katika kata ya msangani ili kuweza kujizatiti zaidi na kukijenga chama kuanzia ngazi za chini hadi za juu.

 

Pia Mbunge huyo katika kukiimarisha chama amegawa bendera na tisheti  kwa mabalozi wote wa mashina yapatayo Saba   yaliyopo katika kata ya msangani.

 

Ziara hiyo ya kamati ya siasa ya chama Cha mapinduzi CCM Kibaha  mji imefanyika katika kata ya msangani na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama hicho imelenga kuwatembelea wanachama wake pamoja na kuzungumza nao juu ya mikakati ya kukijenga chama.

No comments:

Post a Comment

Pages