.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Kyerwa Daniel Damian akitoa maelekezo ya Serikali kwa viongozi wa Halmashauri hiyo.
Na Lydia Lugakila Kyerwa
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera Daniel Damian katika Kikao Cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Daniel amesema kuwa Maagizo ya Chama Cha Mapinduzi yanaelekeza Madiwani kutimiza Majukumu yao katika kutatua kero Sugu bila kujali itikadi za Chama fulani.
"Chama chochote cha Siasa kinatakiwa kuhakikisha kinatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambapo kila Diwani ahakikishe anashughulikia kero zote ili wananchi wasikwame katika shughuli za kimaendeo" alisema Mwenyekiti huyo.
Amesema Chama Cha Mapinduzi hakitamuonea huruma Diwani yeyote atakayeonyesha dalili za uzembe katika eneo lake na kuwa atakayeshindwa kuwajibika katika utatuzi wa Kero Sugu atachukuliwa hatua kisheria.
Katika Hatua nyinginezo Mwenyekiti huyo ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kutoa semina kwa Wakulima waishio Vijijini ili kuwasaidia kupata Hati miliki za Kimila zitakazomruhusu mtu yeyote kwenda popote kukopeshwa katika Taasisi za kifedha na kuendeleza shughuli za kilimo chenye tija.
Aidha ameitaka Ruwasa Wilayani humo kupeleka maji katika Taasisi zote za Kiserikali hasa katika Shule za Sekondari kwa wanafunzi wanaolala shuleni ili kuwanusuru na adha hiyo.
Hata hivyo amempongeza Rais Dkt Samia namna alivyoipendelea Halmashauri hiyo katika Miradi mbali mbali ya Maendeleo.
No comments:
Post a Comment