HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 14, 2023

NSSF yakusanya bilioni 165 Kutokana na vitega UCHUMI vya mfuko

Jasmine Shamwepu, Dodoma


Katika nusu mwaka wa fedha uliyoishia Desemba 2022, mfuko wa NSSF ulikusanya shilingi bilioni 165.7 kutokana na mapato ya uwekezaji na vitega uchumi vya mfuko.


Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Masha Mshomba amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa mfuko huo hapa nchini kwa mwaka wa fedha ulioishia Desemba.


Katika nusu mwaka wa fedha uliyoishia desemba 2022, mfuko  NSSF ulikusanya shilingi bilioni 165.7 kutokana na mapato ya uwekezaji na vitega uchumi vya mfuko.


Aidha Mkurugenzi huyo amesema kiasi hiki cha mapato hakijajumuisha ongezeko la thamani ya vitega uchumi wa mfuko,katika kipindi husika thamani ya vitega uchumi vya mfuko (Investment Portfolio) ilikua na kufikia shilingi trilioni 5.8 ikiwa ni ongezeko la asilimia 7 ukilinganisha na thamani ya shilingi trilioni 5.4 iliyofikiwa katika mwaka wa fedha ulioishia mwezi Juni 2022.


Katika mwaka wa fedha unaoishia Juni 2023 thamani ya vitega uchumi vya mfuko vinatarajiwa kukua na kufikia shilingi trilioni 6.3 ambalo ni ongezeko la asilimia 17 ukilinganisha na thamani ya shilingi trilioni 5.4 iliyofikiwa mwezi Juni 2022.


“Kwa upande wa uwekezaji NSSF tuna fursa za nyumba za makazi salama,kupitia mfuko huu mwananchi anaweza kumiliki nyumba ya ndoto yake kwa kulipa gharama ya nyumba kwa mkupuo mmoja au kulipa kidogo kidogo wakati wakiendelea kuishi katika nyumba husika, nyumba hizi  zipo Dungu,Mtoni Kijichi na Toangoma Jijini Dar es Salaam”Amesema Mshomba.


Katika nusu ya mwaka wa fedha uliyoishia Desemba 2022, mfuko ulilipa mafao ya shilingi bilioni 350.7 kwa NSSF yakusanya bilioni 165 Kutokana na vitega UCHUMI vya mfuko.


No comments:

Post a Comment

Pages