HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 16, 2023

Walanguzi wa Mazao wapewa Onyo

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

Kufuatia kuwepo kwa  vitendo vya ulanguzi usio halali wa mazao kwa wakulima hapa nchini Bodi  ya usimamizi wa Stakabadhi Za Ghala (WRRB) imetoa wito kwa walanguzi wa mazao kuacha kuwalagai wakulima kwa lengo la kujinufaisha. 



Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma  na Mkurugenzi wa Bodi hiyo  Asangye Bangu Wakati akielezea utekelezaji wa bodi hiyo kwa  waandishi wa habari  ambapo amesema  hali hiyo imeifanya Serikali  kuchukua hatua ya kuanzisha mfumo ambao utasaidia kuondoa hali ya sintofahamu kwa wakulima.

Pia amesema Bodi imeweka mikakati ya kuanzisha maghala ya kisasa ya bei nafuu pamoja na kutoa elimu  kwa jamii .

Aidha amesema kumekuwa na wimbi la watu wanaokwenda mashambani kwa wakulima wenye hali ya chini na kununua mazao wa bei ya chini jambo ambalo linamdidimiza mkulima kwa kuwa anatumia nguvu nyingi kulima bila kupata faida inayoendana na nguvu aliyopoteza.

Bangu ametoa wito Kwa madalali waache kuwarubuni wakulima ili wajiunge katika Mfumo wa Stakabadhi ghalani ili waweze kuuza mazao yao kwa bei ya ushindani iliyopo sokoni kwa kuendelea kuuza mazao shambani inaendelea kuwadidimiza wakulima kwa sababu madalali wengi wananunua mazao kwa bei ya chini tofauti kabisa na bei iliyopo kwenye mfumo.

Akieleza  mafanikio yaliyopatikana baada ya kuanzishwa kwa Mfumo wa Stakabadhi za ghalani amesema kuwa  ni pamoja na ongezeko la bei za mazao, mapato ya mkulima na mapato ya Serikali kwa wastani wa asilimia 200% kutokana na urasimishaji,

"Ongezeko la uzalishaji wa mazao kwa wastani wa asilimia 12% kwa mwaka na kichecheo cha ubora wa mazao yanayofikishwa sokoni"amesema Bangu

Bodi ya usimamizi  wa stakabadhi za ghala ni Taasisi iliyopo chini ya wizara ya viwanda na Biashara iliyopewa majukumu ya kutoa leseni kwa waendesha ghala usajili na kuingiza taarifa za wadau muhimu wa mfumo iliyoundwa na sheria namba kumi ya mwaka 2005.


No comments:

Post a Comment

Pages