HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 16, 2023

Wadau wa Maendeleo watakiwa kuoanisha jitihada zao za maendeleo ili kuleta tija kwa wananchi

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wadau maendeleo nchini kuoanisha jitihada zao za maendeleo pamoja na jitihada za Serikali ili kuwa muunganiko wa nguvu katika vipaumbele vya Serikali na kuleta tija kwa wananchi ambao ni wanufaika wa mipango ya maendeleo.


Ameyasema hayo leo  Jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Majadiliano ya Kimkakati  kati ya Serikali  na Washirika wa Maendeleo wenye kauli mbiu “Kuongeza Kasi  ya Kuimarisha Uchumi Himilivu na Jumuishi katika  Nyakati Zisizotabirika ili Kufikia Malengo ya Dira za Maendeleo ya taifa” .

Amebainisha kuwa kulikuwa na malalamiko ya wenzetu ambao tunafanya nao  biashara kuhusu utitiri wa kikodi hivyo ni sehemu ambayo sasa wameshaiangalia ” Rais alivyoingia madarakani alishafuta zaidi ya tozo 114 kwahiyo tunauhakika wa hivyo utaendelea  kuvutia ukiangalia kwenye sekta ya uzalishaji  katika bunge lililopita mheshimiwa rais alifuta kodi na tozo mbalimbali  zinazohusisha sekta hizo lengo  likiwa ni kutengeneza sekta hizo zivutie”. Amesema

Amesisitiza kuwa wamesaini pia mikataba ya makubaliano na nchi mbalimbali kwaajili ya soko la bidhaa kwasababu vilivyokuwa vinavunja moyo kwenye sekta za uzalishaji ni utitiri wa kodi  kwahiyo wamesaini makubaliano  hayo  kwenye masuala ya samaki na maparachichi kwa nchi  mbalimbali  na kusaidia pato la mtu mmoja mmoja kupanda.

Aidha Dkt. Mwigulu ameongeza kuwa lengo la serikali ili kikabiliana na mfumuko wa bei ikiwemo bei za vyakula ni kuongeza uzalishaji wa ndani ili kujitegemea na kuweza kuhimili majanga mbalimbali ikiwemo Uviki19, mizozo ya kivita pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum amebainisha mikakati ya serikali ya Zanzibar katika kukuza uchumi ni uwepo wa sera ya uchumi wa buluu ambapo fursa zilizopo ni ujenzi wa bandari mpya pamoja na teknolojia katika ili kuendana na sera hiyo.

Hata hivyo nao wadau wa maendeleo wamesema dhumuni lao ni kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu mas serikali kwa kuzingatia sera na sheria zilizopo ili kuwa ma uchumi imara na ustawi wa maendeleo ya taifa.

No comments:

Post a Comment

Pages