Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeanza ziara yake
leo tarehe 15 Machi, 2023 katika Wilaya ya Kahama, Mkoani Shinyanga na
kukagua Miradi miwili ya Maji inayosimamiwa na Wakala wa Usambazaji Maji
Vijijini (RUWASA) na Mamlaka ya Maji ya Shinyanga (SHUWASA).
Miradi hiyo iliyokaguliwa yote inapokea maji kutoka mradi mkubwa unaotoka Ziwa Victoria unaosimamiwa na KASHWASA.
Miradi hiyo miwili ni mradi wa Kagongwa - Isaka kwenda vijiji vya Kilimbu, Jana, Butondolo na Itogwanholo.
Mradi mwingine ni mradi wa maji katika Mji wa Tinde na Shelui.
Aidha,
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mheshimiwa
Jackson Kiswaga (Mb) amesema Kamati imetidhishwa na utekelezaji wa
miradi hiyo na kuziagiza RUWASA na Mamlaka ya Maji (SHUWASA) kuangalia
uwezekano wa kuongeza vituo vingine vya kuchotea maji ili wananchi
wapate maji kwa ukaribu zaidi.
No comments:
Post a Comment