HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 09, 2023

KMC FC KUUMANA NA KAGERA SUGAR, UHURU

Na John Richard Marwa

Klabu ya KMC FC, vijana wa Kinondoni leo wanashuka dimbani kuwavaa Kagera Sugar mchezo wa raundi ya 24 Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NBC PL, msimu huu 2022/23.

Mtanange huo utapigwa kwenye Dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam majira ya saa 10 jioni,  ambapo KMC wanaingia kwenye mchezo huo wakihitaji ushindi ili kusogea eneo salama katika msimamo wakati Kagera Sugar wanataka alama tatu wapande nafasi ya tano.


KMC wanashuka dimbani leo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya mechi zake za mwisho ikiwa hawajapata matokeo katika michezo mitatu ya mwisho huku Kagera Sugar wakitoka kushinda mechi mbili na sare moja kwenye mechi zao tatu za mwisho.

No comments:

Post a Comment

Pages