Na Khadija Kalili
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani leo asubuhi Machi 28 wametoa taarifa kwa kipindi cha robo ya Oktoba hadi Desemba mwaka 2022 ambayo imebaini madudu na udanganyifu kwenye Vyama vya Ushirika na Vyama vya Msingi vya Mazao na Masoko (AMCOS).
Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Pwani Christopher Myava amesema kuwa TAKUKURU wamefanya kazi ya ufuatiliaji wa miradi 75 ya maendeleo yenye thamani ya Mil.11,421,038,710.71 katika sekta ya Elimu, Afya, Maji na Barabara ambapo wamebaini kuna upungufu mchache kwenye utekelezaji ikiwa ni pamoja na Shule ya Sekondari Viziwaziwa iliyopo Wilayani Kibaha Mjini wenye thamani ya Mil.470 (470,000,000) mabati yaliyotumika kuezekea jengo la Utawala Maabara, na Vyoo vya Shule. Hayakuwa na kiwango kilichothibitishwa kuezekea majengo ya serikali ambayo ni geji 28 badala yake yalitumika mabati ya geji 30.
"TAKUKURU tumeanza kufanya uchunguzi na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote waliohusika baada ya uchunguzi kukamilika" amesema Kamanda Myava.
Kamanda Myava amesema kuwa ukarabati wa Skimu ya maji Kijiji cha Mkongo Wilayani Rufiji yenye thamani Mil.500 (512,208,249.03), imebainika katika tanki moja la kuhifadhia maji linavujisha pia milango ya jengo la Ofisi ya Jumuia ya watumiaji maji Kijiji TAKUKURU na Ofisi ya Meneja wa Mamlaka ya Usambazaji maji vijijini (RUWASA)tumekubaliana kuwa RUWASA wahakikishe mkandarasi anarekebisha mapungufu yaliyobainika kabla ya muda wa matazamio kuisha" amesema Kamanda Myava.
Akizungumzia kuhusu uchambuzi wa mifumo amesema kuwa ili kudhibiti mianya ya rushwa katika Idara za Serikali na sekta binafsi chambuzi za mifumo tatu zimefanyika kwenye maeneo ya uendeshaji na usimamizi wa masoko ya biashara pamona utekelezaji miradi kwa kutumia 'force account' katika Vyama vya Ushirika vya msingi vya mazao na masoko (AMCOS) vya Mkongo Kilimani ,Kitupa, Nyaminywili, Kipo na Ngorongo AMCOS zote za Wilayani Rufiji Mkoani Pwani.
Amesema kuwa katika uchambuzi huo wamebaini kuwepo kwa udhaifu katika utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu za Vyama vya Ushirika ambapo baadhi ya nyaraka zimekuwa zikitunzwa nyumbani kwa viongozi wa bodi huku akiitaja AMCOS ya Kipo kuwa baadhii ya nyaraka zake zimeonekaba kuharibiwa na mchwa.
"Hatua hii ya kukosa kumbukumbu ya nyaraka zilizoharibika imesababisha changamoto katika kubaini mapato na matumizi ,takwimu na taarifa zote za fedha kwa ujumla" amesema Kamanda huyo.
Aidha ameweka wazi kuwa maazimio yaliyowekwa ni kuwa ujenzi wa Ofisi bora ya kutunza nyaraka na kumbukumbu za Ushirika uwe umekamolika ifikapo mwaka 2024.
Kuandaa taarifa za fedha na kujaza taarifa sahihi katika nyaraka zote za Ushirika na kuhakikisha zinatunzwa vizuri ikiwa ni pamoja na kununua bomba la kupulizia dawa za wadudu waharibifu.
"TAKUKURU tumebaini kuwa upo udanganyifu wa kutoandika idadi ya kilo sahihi kulingana na mzigo wa mkulima wakati wa upimaji kwa kisingizio cha ubora na unyaufu, mfano.mwananchi anafika na kilo 30.5 lakini kwa makusudi ya kufanya udanganyifu wapimaji ambao ni wajumbe wa Bodi ya AMCOS husika wanamwambia mkulima mazao yako hayana ubora hivyo badala ya kilo 30.5 tutakuandikia kilo 29."
Hali hii ikiendelea kwa wakulima zaidi wajumbe hao watajikusanyia kilo nyingi kwa udanganyifu nakutengeneza mauzo kwa majina hewa kwa manufaa yao, wananchi wanapogundua udanganyifu huu huacha kuuza mazao kwenye AMCOS zao na kwenda kuuza AMCOS za Kata jirani jambo ambalo AMCOS mama zinakosa mapato lakini pia wananchi wanalazimika kutafuta huduma hii.
" TAKUKURU tumechukua hatua za kuwataka kuongeza matumizi ya mizani ya kidigitali na kupunguza matumizi ya mizani ya kusogeza ,pia mazao yenye ubora yasichanganywe ili wakulima wapate madaraja stahiki" amesema Kamanda Myava.
Ameongeza kwa kusema kuwa wametoa maelekezo ya kuandaliwe daftari rasmi la mapokezi ambalo wajumbe wa Bodi watakuwa wakilihakiki na kusaini kila tarehe ya mapokezo ya mazao.
Imebainika kuwa AMCOS ya Mkongo ya Rufiji kutotoa stakabadhi kwa wakulima mara baada ya kupokea mzigo baadaye wakulima hupewa stakabadhi zilizoandikwa kiasi cha kilo yofauti na kile kilichoandikwa awali wakati wa kupokea mzigo hali hii hutengeneza mianya ya rushwa kwa hao wajumbe wa bodi wasio waaminifu wanaopima mazao kutoka kwenye kilo zile walizowapunja wakulima na kutengeneza mauzo kwa faida yao hivyo kusababisha hasara kwa Ushirika na wakulima.
"Tumebaini kuwa matumizi ya skabadhi za kuandika na mkono badala ya POS kukusanyia ushuru ambazo pia wakati mwingine hazitolewi baada ya malipo kufanywa mfano soko kuu la Mji wa Utete, soko la Kijiji Ikwiriri ukusanyaji wa mapato bila kutoa skakabadhi ya mashine POS kwa kisingizio cha ubovu wa mashine hali inayosababisha upotevu wa mapato yanayokusanywa ikiwemo soko la Mnarani Wilayani Kibaha wafanyabiashara waliohojiwa baadhi wamedai kutopatiwa skakabadhi za malipo kutoka kwa wakusanya ushuru.
Hivyo basi tumeagiza kuongeza ufanisi wa matumizi ya POS katika kukusanya ushuru ili kuongeza mapato,ikiwemo kufanha ukaguzi wa mara kwa mara ili kuongez usimamizi kwa wakusanya ushuru kwa lengo la kudhibiti.ukusanyaji mapato.
Mwisho Kamanda Myava ametoa wito wa TAKUKURU kwa wananchi na wadau wote katika Taasisi za serikali nansekta binafsi kuunga mkono program ya TAKUKURU RAFIKI kwani inahusisha jitihada za kutambua na kutatua kero zinazoweza kusababisha uwepo wa vitendo vya rushwa kama zitaachwa bila kushughulikiwa kwenye sekta za maji, elimu, nishati (Umeme), afya, barabara, ardhi, huduma za jamii na miradi ya maendeleo inayotekelezwa ba serikali, utatuzi wa kero zitakazoibuliwa kupitia programu hii unatarajjwa kuimarisha utoaji huduma ,kuboresha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ,kuimarisha uzingatiaji wa misingi ya Utawala Bora na kupunguza vitendo vya rushwa
No comments:
Post a Comment