HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 21, 2023

Watafiti watakiwa kuhakikisha tafiti zao zinawafikia watumiaji

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinwarakiwa yi amewahimiza watafiti kuhakikisha tafiti zao zinawafikia watumiaji.


Pia Dk. Mwinyi alishauri matokeo ya utafiti yawafikie watunga sera ili wayatumie kwa utungaji wa sera bora.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo kwenye hafla ya kusambaza matokeo ya tafiti za UVIKO-19 zilizofanywa na chuo Kikuu cha MUHAS kupitia ufadhili wa familia ya Hayati Amne Salim hafla iliyofanyika kwenye jengo la CHPE, kampasi ya Muhimbili Dar es Salaam.

Dk. Mwinyi aliwataka wataalam wa ndani kuyapokea matokeo ya utafikti huo na
 kuyafanyiakazi, ili kuongeza kasi ya udhibiti wa maambikizo ya UVIKO -19 nchini.

Alieleza tafiti hizo zimeonesha namna za athari za ugonjwa huo na kuongeza kuna mafunzo yakitumiwa vyema yatasaidia mapambano sio tu ya UVIKO  bali pia kwa magonjwa mengine.

"Bila shaka ushauri WA kisayansi unaweza kuwa na tija zaidi ikiwa utatumika kwa wakati na sio kukaa kwenye majarida ya kimataifa peke yake" Alishauri Dk. Mwinyi.

Alisema msaada uliotolewa na familia ya Hayati Mama Amne Salim, Mke wa Dk. Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania unakumbusha jukumu la kila Mtanzania popote alipo kwa namna yake kuona anamchango kwa taifa lake.

"Kwa utaratibu huu tunaweza kwenda mbali zaidi na kupambana na hatari yoyote" Alieleza Dk. Mwinyi.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo, kuipongeza familia Hayati Mama Amne Salim kwa niaba ya serikali zote mbili za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Pia Dk. Mwinyi alikipongeza Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa kuutendea haki ufadhili huo na kueleza kuwa taasisi ya MUHAS ilihakikisha Fedha zilizotolewa kwaajili ya utafiti huo shilingi milioni mia moja na tano zilitumika kwenye utafiti huo.

"Nawapongeza MUHAS kwa weledi na uadilifu wenu, utaongeza fursa zaidi za ufadhili wa utafiti kutoka kwa Watanzania wengine" Alipongeza Dk. Mwinyi.

Pia Dk. Mwinyi aliwawapongeza wanasayansi wa MUHAS na Watanzania kwa ujumla kwa kazi nzuri wanazoendelea kuzifanya na kusifu kufarajika kwake kwa chuo cha MUHAS  kuwa cha kwanza Afrika Mashariki na Kati kufanya tafiti nzuri na machapisho.

Alieleza kwamba anatarajia tafiti hizo zitaleta unafuu kwa wananchi kwa kutatua changamoto zinazoijabili jamii ili kufikia malengo endelevu nchi iliyojipangia.

Mapema Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda, aliwataka wadau wajitokeze kufanya tafiti mbalimbali na waunge mkono kazi iliyofanywa  na Dk. Salim Ahmed Salim pamoja na familia yake.

Pia alibainisha Serikali imetenga shilingi milioni 50 kwa kila utafiti utakaofanywa na machapisho yake yakichapishwa sehemu mbalimbali duniani. IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

Pages