HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 03, 2023

MWIJAKU ATANGAZWA KUWA MWENYEKITI WA CHAWA MAMA DAR

 Na Khadija Kalili


MTANGAZAJI  maarufu wa Kituo Cha Redio kongwe nchini   Clouds FM Mwemba Burton   almaarufu kama Mwijaku  ametangazwa kuwa Mwenyekiti wa Chawa wa Mama  Mkoa wa Dar    es Salaam .



Katibu wa Chawa wa Mama Taifa Neema  Karume amesema kuwa  uteuzi  huo umekuja baada ya Mwijaku  kukidhi vigezo vya kuwa na nguvu ya uhamasishaji  katika masuala ya Chama na Serikali na jamii nzima kwa ujumla.


Uteuzi huo umefanyika Aprili Mosi mwaka 2023  Jijini Dar es Salaam .

"Tunamkaribisha  sana ili tuungane kwa pamoja kuyasema yale yote mazuri anayoyafanya Rais wetu mpendwa Dkt.Samia Suluhu Hassan hakika mama amefanya makubwa hatuna budi kumuunga mkono katika juhudi zake  zote" amesema Katibu wa Chawa wa mama Taifa  Neema Karume.

 

Katibu huyo  wa Chawa Taifa Neema  ameongeza kwa kusema kuwa kundi  la Chawa wa Mama linaundwa na watu kutoka kada mbakimbali nchi nzima huku akiyataja baadhi yao makundi hayo kuwa  ni Madereva wa Bodaboda ,  Madereva Taxi, Mabasi ya Abiria, Mama Lishe ,Wakulima, Wafugaji,Wafanyabiashara wakubwa na Wamachinga, Wasusi, Wavuvi, Wanasiasa, Wanafunzi wa Vyuo, Waalimu, Wakurugenzi katika taasisi mbalimbali  Wafanyakazi wa Serikali na Taasisi  binafsi  na Watanzani waliopo nje ya nchi ( DIASPORA).


Neema amesema kuwa lengo la kundi la  Chawa wa Mama ni kuhakikisha  wanakuwa  Mabalozi  wazuri  ndani na nje  ya nchi  kwakuyasemea yake mazuri  yanayotekelezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na  kuhakikisha  ifikapo  mwaka 2025 wanaweka historia kwa  Rais Dkt. Samia Hassan kuliongoza taifa katika awamu ya saba.


Amesema kuwa Mwijaku amechaguliwa baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Jiji  la Dar es Salaam Diwani wa Viti Maalumu Beatrice  Nyamisago  ambaye pia ni Afisa  Habari  Chawa wa Mama Taifa kuamua kuachia nafasi hiyo .


"Nyamisago ameona si vema  kushikilia nafasi mbili  hivyo  ameomba ang'atuke katika nafasi ya Mwenyekiti wa Dar Es Salaam" amesema Neema. 

No comments:

Post a Comment

Pages