Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dk.Aneth Komba amewataka walimu kuhakikisha wanatumia vitabu vya kiada na ziada vyenye ithibati ya Kamishna wa Elimu.
Hayo ameyasema leo Machi 03, 2023 Jijini Dodoma katika ufunguzi wa mafunzo endelevu ya walimu kazini ya Elimu ya Awali (Watoto Wetu Tunu Yetu) kwa Walimu na Viongozi wa Elimu yanayotelewa na Shirika la "Children in Crossfire"
"Walimu ni chachu ya mabadiliko katika Elimu hivyo nawasisitiza matumizi ya vitabu vya kiada na ziada vilivyo na ithibati ya Kamishna wa Elimu, ni muhimu sana kutumia vitabu hivi kwani kuna vitabu vingi huko mtaani vyenye maudhui ambayo hayaendeni na tamaduni zetu, nasisitiza kila shule itumie vitabu vyenye ithibati katika kufundisha na kujifunza" amesema Dk.Aneth.
Aidha,amewaelekeza walimu hao kutumia Maktaba mtandao ya TET ambayo ina vitabu vyote vya kiada na ziada, miongozo, mihtasari na mitaala.Ameeleza kuwa Maktaba hiyo kwa sasa inapatikana bure kwa mtumiaji mwenye laini ya simu ya Airtel na wapo katika mchakato wa kuongea na kampuni nyingine za simu ziweze kutoa huduma hiyo bure.
Awali, alishukuru shirika la Children in Crossfire kupitia mradi wa "Watoto Wetu Tunu Yetu" kwa kuendelea kuwa wadau muhimu katika elimu hususani elmu ya Awali katika kuboresha mazingira ya ujifunzaji .
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika la "Children in Crossfire"Bwana.Heri Ayubu amesema kuwa mradi huo wa
"Watoto Wetu Tunu Yetu"unatekelezwa katika mikoa mitatu (Mwanza, Morogoro na Dodoma)
Ukiwa na lengo la kuendelea kuchangia uboreshaji wa utoaji wa elimu ya Awali nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Serikali.
Amesema kuwa,mwisho wa mradi huo wanatarajia kuona ongezeko kubwa la wanafunzi wenye utayari wa kuingia darasa la Kwanza.
Mafunzo hayo yanawashirikisha walimu wa darasa la awali,maafisa elimu,wadhibiti ubora,maafisa taluma kutoka wilaya za Mpwapwa, Bahi na Dodoma Jiji.
No comments:
Post a Comment