HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 02, 2023

CRDB yatangaza matokeo Programu ya Imbeju, Biashara 196 zafuzu


Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo, akizungumza na waandishi wa habari  wakati wa mkutano wa kutangaza matokeo ya Programu ya Imbeju ambapo 
biashara 196 zilipitishwa kuendelea hatua inayofuata. Mkutano huo ulifanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo Mei 2, 2023.  (Picha na John Dande).

Mkurugenzi wa Usanifu  na Teknolojia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dk. Gerald Kafuku, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.





 

UZINDUZI NA UFUNGUZI WA DIRISHA LA MAOMBI

 

Ndugu Waandishi wa Habari, Kama mnavyofahamu tarehe 12 Machi mwaka huu Benki yetu ilizindua rasmi program ya IMBEJU iliyobeba kaulimbiu ya “Mtaji Wezeshi kwa Vijana na Wanawake” ambayo inatekelezwa kupitia taasisi yetu ya CRDB Bank Foundation.

 

Uzinduzi ule ulienda sambamba na ufunguzi wa dirisha la maombi upande wa biashara changa bunifu za vijana (Startups), na biashara changa za wanawake kupitia vikundi. 
 


Kipekee kabisa nimshukuru Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kutupa heshima ya kutuzindulia na kutufungulia dirisha la maombi kwa vijana na wanawake. 
 


MAOMBI YA BISHARA CHANGA BUNIFU ZA VIJANA

 

Ndugu Waandishi wa Habari, Ufunguzi wa dirisha la maombi ulikuwa ni hatua ya kwanza ya utekelezaji wa program ya IMBEJU ambayo inahusisha mafunzo, ushauri, na utoaji wa mitaji wezeshi.


 

Kwa upande wa biashara changa bunifu za vijana tunayofanya na washirika wetu wa COSTECH na ICTC, dirisha lilifunguliwa kwa muda wa mwezi mmoja na kufungwa Aprili 12, 2023. 

 

Katika kipindi cha mwezi huo mmoja, vijana walipewa fursa ya kuwasilisha maombi ya ushiriki katika programu ya IMBEJU kupitia tovuti za COSTECH na ICTC. 


 

Ninapenda kuwajulisha kuwa hadi Aprili 12 ambapo dirisha la maombi lilifungwa, jumla ya maombi 709 yalipokelwa 369 kupitia COSTECH, na 340 kupitia ICTC. 


Maombiyalipokelewa kutoka mikoa yote, ambapo katika maombi  hayo  yaliyo wasilishwa asilimia 70.6 ni vijana wa kiume na asilimia 29 ni wa kike. 


Kwa upande wa maombi yaliyowasilishwa kupitia COSTECH, nafurahi kuwajulisha kuwa sekta ya kilimo ambayo ni utiwa mgongo wa Taifa letu imeongoza kwa kuwa na asilimia 31 ya maombi yote ikifuatiwa na sekta ya uzalishajiyaani “manufacturing” ikiwa na asilimia 14. 
 


Kwa upande wa maombi yaliyowasilishwa kupitia ICTC, nafurahi kuwajulisha kuwa sekta ya biashara ya mtandaoni yaani“e-commerce” imeongoza kwa kuwa na asilimia18 ya maombi yote ikifuatiwa kwa karibu na sekta ya teknolojia ya masuala ya fedha yaani “Fintech” ikiwa na asilimia 13. 


UCHAKATAJI WA MAOMBI

 

Ndugu Waandishi wa Habari, Baada ya kupokea maombi hatua ya pili ilikuwa kuyachakata ambapo timu mbili ziliundwa zikijumuisha wataalamu kutoka Benki ya CRDB, COSTECH na ICTC kwa kuzingatia vigezo vya programu. 


 

Ninapenda kuwajulisha kuwa jumla ya biashara 196 zilipitishwa kuendelea hatua inayofuata, kutoka COSTECH zilikuwa 116 na ICTC 80. 
 


Majina ya waliyofanikiwa kupita katika hatua inayofuata yamewekwa katika tovuti za COSTECH na ICTC. Kipekee kabisa nichukue fursa hii kuwapongeza waliochanguliwa kwenda hatua inayofuata ya mafunzo.


 

Kwa ambao hawajafanikiwa niwasihi wasikate tamaa kwani programu ya IMBEJU niendelevu, hivyo wajipange kwa dirisha lijalo. 

 

Lakini, kutochaguliwa kwao kwenda hatua inayofuata sio kwamba tunawaacha hivihivi,Benkiinawapa fursa ya kufungua akaunti ya IMBEJU yenye faida lukuki zitakazo wasaidia kusimamia vizuri biashara zao ikiwamo mifumo ya malipo na bima ya biashara, na maisha. 


HATUA INAYOFATA BAADA YA KUCHAKATA MAOMBI 

 

Ndugu Waandishi wa Habari, Zoezi lililofanyika lilikua ni mchakato wa awali wa kupitia maombi ili kutambua yale yaliyokidhi vigezo vya awali kabla ya kwenda katika hatua inayofuata.

 

Hivyo baada ya zoezi hili kukamilika zoezi linalofata ni uchakataji wa maombi yaliyofaulu katika hatua ya kwanza ambapo katika hatua hiyo tutakwenda kukutana na wahusika na kupata maelezo ya kina ya maombi yao ilikujiridhisha kuwa kile tulichokisoma na wanachokizungumza wao wenyewe vinaendana.

 

Sambamba na kukutana nao lakini pia tutakwenda kuhakiki masuala mbalimbali yanayohusiana na maombi yao ikiwemo masuala ya hatimiliki ili kuhakikisha kuwa mawazo yaliyowasilishwa hayajachukuliwa kwa watu wengine ambao tayari wana umiliki nayo. 
 


Hivyo katika hatua hii ya pili, mbali na ICTC na COSTECH vile vile tutakua na COSOTA ambayo ni taasisi ya Serikali inayosimamia masuala ya hatimiliki. 


Lakini pamoja na taasisi hizi pia tutakua na wakaguzi huru ‘independent audit firm’ ambayo itahakikisha taratibu zote zinazingatiwa. 
 


Niwaombe vijana wote waliochaguliwa wafuatilie kwa ukaribu taarifa zitakazokuwa zikitolewa na kutumwa moja kwa moja kwao juu ya lini watahitajika kwa ajili ya hatua ya pili ya uchakataji wa maombi.

 

Tunatarajia hatua hiya pili ya uchakataji wa maombi kukamilika ndani ya wiki mbili hadi tatu zijazo ambapo tutawaita tena na kuwapa taarifa juu ya hatua hiyo.

 

BIASHARA ZA WANAWAKE KUPITIA VIKUNDI


Ndugu Waandishi wa Habari, Najua mtakuwa mna shauku ya kutaka kufahamu hatua tuliyofikia upande wa biashara za wanawake. 

 

Kwa upande huu bado dirisha lipo wazi na tunaendelea kutoa hamasa kwa vikundi vya wanawake kujiunga katika programu.

 


Mpaka sasa tumeshavifikia vikundi Zaidi ya 200 vya akina mama kupitia matawi yetu kote nchini. Vikundi hivi viko katika mchakato wa kupata mafunzo na kuunganishwa na akaunti ya IMBEJU kisha kupewa mitaji wezeshi. 


 

Tunafahamu kuwa idadi ya wanawake nchini ni kubwa, wanawake ndio wabeba uchumi na ndio asilimia kubwa ya wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo. 


Idadi hii ambayo imefikiwa ni kubwa lakini bado haiendani na wingi wa wanawake na lengo letu ni kumuinua mwanamke wa Kitanzania ndio maana bado hatujatangaza kufunga dirisha.

 

Nitoe rai kwa  wanawake  kote nchini kuchangamkia fursa hii ya program ya IMBEJU ili kuboresha na kukuza biashara zao. 


 

Jipangeni kama kikundi, viongozi wafike tawini kuwasilisha maombi, mtapewa mafunzo, kuunganishwa na Akaunti ya IMBEJU kisha kupewa mitaji ya kuinua bishara zenu.


No comments:

Post a Comment

Pages