HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 06, 2023

OCODE YAZINDUWA RIPOTI YA STADI ZA MAISHA NA MAADILI KWA VIJANA WILAYA YA KINONDONI

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Given Sure (kushoto) kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa –RAS, akizindua rasmi ripoti ya tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) katika Wilaya ya Kinondoni. Wanaoshiriki ni Mkurugenzi Mtendaji wa Organization for Community Development (OCODE), Joseph Jackson (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati za Shule zilizo chini ya Miradi ya OCODE, Bw. Hamza Mirambo.

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Given Sure (kushoto) kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa –RAS, akizindua rasmi ripoti ya tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) katika Wilaya ya Kinondoni. Wanaoshiriki ni Mkurugenzi Mtendaji wa Organization for Community Development (OCODE), Joseph Jackson (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati za Shule zilizo chini ya Miradi ya OCODE, Bw. Hamza Mirambo.

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Uwezo Tanzania, Bw. Greyson Mgoi akitoa taarifa juu ya Mradi wa tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) katika Wilaya ya Kinondoni kwenye hafla ya uzinduzi wa ripoti ya ALiVE Wilaya ya Kinondoni iliyofanyika Ukumbi wa Ngome Holdings jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Tathmini wa Stadi za Maisha na Maadili (ALiVE) Wilaya ya Kinondoni, Bi. Tunu Sanga akitoa matokeo ya tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) katika Wilaya ya Kinondoni kwenye hafla ya uzinduzi wa ripoti ya ALiVE Wilaya ya Kinondoni iliyofanyika Ukumbi wa Ngome Holdings jijini Dar es Salaam.

Washiriki katika hafla ya uzinduzi wa matokeo ya tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) katika Wilaya ya Kinondoni iliyofanyika Ukumbi wa Ngome Holdings jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada anuai.


Mratibu wa Tathmini wa Stadi za Maisha na Maadili (ALiVE) Wilaya ya Kinondoni, Bi. Tunu Sanga akisisitiza jambo katika hafla hiyo.

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Given Sure (wa pili kushoto) kwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Organization for Community Development (OCODE), Joseph Jackson, Mwenyekiti wa Kamati za Shule zilizo chini ya Miradi ya OCODE, Bw. Hamza Mirambo na Mratibu wa Tathmini wa Stadi za Maisha na Maadili (ALiVE) Wilaya ya Kinondoni, Bi. Tunu Sanga wakionesha nakala ya ripoti hiyo mara baada ya kuzinduliwa.

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Given Sure kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa –RAS, akizungumza mara baada ya kuzindua ripoti ya tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) katika Wilaya ya Kinondoni. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Organization for Community Development (OCODE), Joseph Jackson akifuatilia.

Mmoja wa vijana wanufaika na miradi ya OCODE akielezea namna ilivyomnufaisha.

Sehemu ya washiriki katika hafla ya uzinduzi wa matokeo ya tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) katika Wilaya ya Kinondoni iliyofanyika Ukumbi wa Ngome Holdings jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada anuai.

Washiriki katika hafla ya uzinduzi wa matokeo ya tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) katika Wilaya ya Kinondoni iliyofanyika Ukumbi wa Ngome Holdings jijini Dar es Salaam wakifuatilia uzinduzi huo.

Mdhibiti Mkuu Ubora wa Shule Kinondoni, Bi. Naitwa Mgumba akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa ripoti ya ALiVE Wilaya ya Kinondoni iliyofanyika Ukumbi wa Ngome Holdings jijini Dar es Salaam.


RIPOTI ya tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) katika Wilaya ya Kinondoni imezinduliwa rasmi na Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Given Sure kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa –RAS. 

Uzinduzi wa ripoti hiyo ya kupima tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) ya vijana umefanyika katika Ukumbi wa Ngome Holdings jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na washiriki katika hafla ya uzinduzi wa matokeo ya tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) katika Wilaya ya Kinondoni, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Given Sure kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa, aliitaka jamii kubadilika katika mtizamo wa malezi ndani ya familia.

Alisema ipo haja ya kuanza kuwaandaa vijana wetu kuanzia ngazi ya familia, kwa sababu vijana wanaanza kujifunza maadili kuanzia ngazi ya familia.

”…Mfano mzuri wa baadhi ya wazazi kujisahau katika kuwajenga vijana unaweza kukuta mzazi anaona taa imesahaulika inawaka bila matumizi sahihi mzazi badala ya kumwambia mtoto wake akazime taa hiyo anamuita binti wa kazi ndio anampa maelekezo ya kuzima taa hiyo, sasa huku ni kujisahau kimalezi katika kuwajenga vijana kuanzia ngazi ya familia…,kimsingi mzazi unapaswa kuanza kumwambia mtoto wako kwanza,” alisema Bi. Sure.

Alisema tunu za maadili na kujielewa kwa vijana inapaswa kuanzia katika ngazi ya familia na kupanda juu ili kuwaandaa vijana kujitambua.

Awali akisoma matokeo ya taarifa hiyo, Mratibu wa Tathmini wa Stadi za Maisha na Maadili (ALiVE) Wilaya ya Kinondoni, Bi. Tunu Sanga alibainisha kuwa jumla ya vijana 363 wa kuanzia miaka 13 hadi 17 kutoka katika kaya 322 walifanyiwa tathmini ya stadi za maisha na maadili (ALiVE) huku ikionesha ni vijana 6 kati ya 10 wenye uwezo wa kutatua matatizo yao.

Katika kujitambua na kujidhibiti ni vijana 6 kati ya 10 walionesha kujitambua, na katika kujitambua na kimtizamo ni vijana 7 kati ya 10 walionesha kumudu hali hiyo. Aliongeza kuwa katika tunu ya heshima ni vijana 6 kati ya 10 ndio waliomudu tunu ya maadili.


No comments:

Post a Comment

Pages