HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 05, 2023

TIMU YA TAIFA U 18 NA 20 KUPASHA MBEYA TULIA MARATHON 2023

MSAFARA wa Timu ya Taifa ya Riadha kwa vijana chini ya miaka 18 na 20, iliyokuwa ikishiriki mashindano ya Afrika huko Ndola,  Zambia na kufanikiwa kupata medali mbili, imewasili jijini Mbeya, leo Mei 4.



Timu hiyo ilifanikiwa kutwaa medali ya Fedha kupitia kwa Mwanaamina Hassan Mkwayu kwenye kurusha Mkuki na Samir Sululu kurusha Tufe.

Kwa matokeo hayo, Tanzania imefanikiwa kushika nafasi ya 12 kwa U 20 na 15 kwa U 18 katika matokeo ya jumla.

Baada ya kuwasili salama Mbeya, timu imepumzika na Mei 5 baadhi ya wachezaji watapata nafasi ya kushiriki mbio za uwanjani Mbeya Tulia Marathon, kabla ya kuendelea na safari ya kurejea jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Pages