HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2023

Aga Khan Foundation yazitaka Taasisi za Kifedha kutoa elimu ya mikopo kwa vijana

Na Hussein Ndubikile, Da es Salaam

Taasisi  zinazotoa mikopo hapa nchini zimetakiwa kutoa elimu ya biashara na mikopo kabla ya kutoa mikopo kwa vijana ili waweze kujiajiri na kukuza biashara zao.

Akizungumza katika Kongamano la Uwezeshaji Mikopo kwa Vijana lililoandaliwa na Taasisi ya Aga khan Foundation (AKF) Meneja Miradi wa taasisi hiyo Simon Meigero amesema kuwa taasisi hiyo imelenga kukuza uwezo wa vijana katika kujiajiri na kukuza uchumi wa nchi.

Aidha amesema kumekuwa na tatizo kwa mikopo mingi ya vijana kutorudi pindi wanapoomba mikopo hiyo jambo ambalo linatokana na kutokuwepo kwa elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya fedha za mikopo na urejeshwaji wake.

“Mpango wa utoaji wa elimu ya biashara na mikopo ni muhimu sana na kwa sasa tunaendelea kutoa elimu hiyo na itajumuisha mikoa ya Mwanza ,Lindi, Dar es Salaam na Mtwara” Amesema Bw. Meigaro.

Kwa upande wake, Katibu wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng'i Issa amesema kuwa kumekuwa na mwamko mdogo kwa wanawake katika kufanya biashara sambamba na matumizi madogo yakufanya biashara mtandaoni hasa kwa wanawake waliopo katika maeneo ya vijijini.

Amesema utaratibu wa kupata mikopo kwa wanawake kutoka Halmashauri nilazima wanawake hao wakajiunga kikundi kisichopungua watu watano na kuwa na akiba kwenye akaunti hivyo mwamko kuwa mdogo katika matumizi ya teknolojia katika kufanya biashara.

No comments:

Post a Comment

Pages