HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2023

Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kusafirsha dawa ya kulevya aina ya bangi

 Na Janeth Jovin,  Dar es Salaam


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kibaha imemuhukumu Abubakar Mbanje kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa kilo 38.84.


Hukumu hiyo ilitolewa juzi kufuatia shauri la jinai namba 37 la mwaka 2022  lililokiwa mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Salumu Ally kumalizika na mtuhumiwa huyo kukutwa na hatia ya kutenda kosa hilo.


Mtuhumiwa alikamatwa  na Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Mei 19, 2022 katika eneo la bandari bubu iliyopo Mlingotini - mji mpya wilaya ya Bagamoyo akiwa na kilo hizo 38.84 za dawa ya kulevya aina ya bangi alizokuwa akizisafirisha kwa kutumia pikipiki.



Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili Rachel Morgan na Gloria Simpassa mawakili wa Serikali na jumla ya mashahidi sita wa upande wa huo walitoa ushahidi wao katika kuthibitisha kosa la mtuhumiwa la kusafirisha sawa hizo za kulevya.


Aidha na upande wa utetezi uliwakilishwa na Wakili Iddi Msawange ambapo ulileta mashahidi wanne akiwemo mshitakiwa mwenyewe.


Hata hivyo baada ya kutiwa hatiani mshtakiwa aliiomba mahakama imuonee huruma na kumuachia huru.



Akisoma hukumu hiyo Hakimu Salumu alisema ametoa adhabu hiyo kwa mshtakiwa kwa mujibu wa sheria na pia ili iwe fundisho kwa wote wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.


Pamoja na hukumu hiyo Hakimu Salumu alitoa amri ya kutaifisha pikipiki iliyotumika kitenda kosa hilo na pia kielelezo ambacho ni dawa za kulevya aina ya bangi kiteketezwa.


No comments:

Post a Comment

Pages