HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 07, 2023

DCPC yaitaka TRA kudhibiti magendo

 

Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanznia (TRA), Richard Kayombo, akifungua mafunzo kuhusu masuala ya kodi kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.


 Kaimu Mwenyekiti wa
Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam DCPC, Tausi Mbowe, akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

 Afisa Mkuu Msimamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Hamad Mterry akitoa mada.


 

Na Mwandishi wetu

KLABU ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dar es salaam DCPC imeishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuongeza nguvu kudhibiti mizigo na biadhaa za magendo inayoingia nchini kinyemela kwasababu inaikoseshea serikali mapato stahiki na kuchelewesha

DCPC imeishauri TRA juzi wakati wa mafunzo kuhusu  Masuala mbalimbali yanayohusu kodi ambapo katika mafunzo hayo klabu inaona ipo haja ya kuongeza nguvu ya udhibiti wa magendo yanayongia nchini kinyemela kwakuwa yanakwamisha juhudi za ukusanyaji wa mapato

Ofisa Mwandamizi na Usimamizi wa Kodi upande wa Forodha TRA Julieth Kidemi alisema miongoni mwa bidhaa zinazoongozwa kuingizwa kinyemela ni pamoja na bidhaa za sukari, sabuni, vitenge ma mitumba hivyo kuna haja ya kushirikiana kikamilifu kudhibiti mianya hiyo

Mkurugenzi wa huduma na Elimu Kwa mlipa Kodi Richard Kayombo  alisema malengo ya ukusanyaji wa Kodi Kwa mwaka wa fedha 2022-2023 ni zaidi ya sh. tirilioni 23 na mpaka kufikia tarehe 31 mwisho wa mwezi huu wa sita makwngo tarajiwa yatakuwa yamefikiwa

Ofisa Mkuu na Usimamizi wa Kodi TRA Hamad Mteri aliwataka wafanyabishara kuzingatia sheria za na kujiepusha na ukwepaji Kodi kinyume chake watakumbana na mkono wa sheria.

Pamoja na mambo mengine mamlaka ya mapato Tanzania TRA inakusudia kuongeza nguvu katika eneo la digitali ili Kuboresha huduma za ukusanyaji wa mapato na kudhibiti magendo
 

 

 


No comments:

Post a Comment

Pages