HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 21, 2023

DIWANI LYOTO AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

Diwani wa Kata ya Mzimuni - Magomeni Mkoa wa Dar es Salaam, Manfred Lyato akizungumza katika mkutano wa hadhara kusikiliza kero za wananchi katika mtaa Idrisa.
Wananchi wa Mtaa wa Idrisa wakimsikiliza Diwani Lyoto.



Na Magrethy Katengu

 

Diwani wa Halmashauri ya Kinondoni  kata ya Mzimuni- Magomeni Mkoa wa Dar es salaam Manfred Lyato amefanya mikutano ya hadhara kusikiliza kero za Wananchi katika mitaa ikiwemo Idrisa na Mwinyimkuu ili kusaidia kero zao  kutatuliwa kwa wakati


Wakitoa kero zao kwa Diwani huyo Mkazi wa Idrisa  Selemani Ally amesema katika Mtaa wanaofanyia biashara kuna Mfereji ambao ni kero kubwa sana kwao maji machafu yamejaa sana na kipindi cha mvua ya hujaa na kuingia katika makazi ya watu hivyo wamemuomba Diwani huyo kuwasaidia kwani Afya zao ziko hatarini ..

Naye Mkazi wa Mtaa wa Idrisa Nasri Ahmadi amesema kero wanayokumbana nayo ni barabara ya mtaa wa  Makumbusho hali ya barabara hiyo ni tope hasa kipindi cha mvua hakupitiki maji ya matope yamejaa na watembea kwa miguu wakipita huchafuka licha ya kila mwaka kumwagwa kifusi iwe juu lakini mvua zikinyesha tu hali huwa mbaya hivyo wanamuomba Diwani huyo ijengwe kwa kiwango cha lami.

Naye Martha Ayubu alitoa kero kwa kusema kuwa wanachangishwa fedha za takataka lakini gari huchelewa kuja kubeba taka na zinakaa zaidi ya miezi mitatu pia akasema kero nyingine ni suala la vitambulisho vya uraia NIDA ni changamoto kwani namba inatoka vitambulisho kila wakifuatilia humbuwa bado kuna tatizo gani hiyo


Akijibu maswali ya Wakazi hao Diwani Kata ya Mzimuni Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam Manfred Lyoto amsema bajeti ya serikali inayokuja ni ndogo haiwezi kutatua changamoto zote hivyo wakati mwingine kiongozi hutoa fedha zake mfukoni kutatua kero za wanancho kwani kama yeye amepanga kuja na Mpango mkakati wa kuanzisha Miradi mbalimbali ukiwemo Mradi wa Kilimo ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa bajeti.


“Kata yetu inachangamoto nyingi ikiwemo sekta ya Elimu, afya, miubdombinu na Bajeti ya Serikali inayotolewa kila mwaka haitoshi, mimi na timu yangu  tumeandaa Mpango mkakati wa kuanzisha miradi itakayotuongezea Mapato na kutatua changamoto katika Kata yetu,” amesema Lyoto.

Hata hivyo amesema miradi waliyopanga kuanzisha kabla ya kumaliza uongozi wake vyo ni Mradi  kilimo utakuwa Mkoani Njombe na Vijana wa Kata ya Mzimuni ndio watakaohusika ikiwa ni sehemu ya kuwapa ajira hivyo amewasihi wawe waaminifu watakapochaguliwa kwenda kufanya kazi na kusimamia mradi

Sanjari na hayo amesema Mradi utakapeta matunda mazuri fedha zitakazopatikana zitasaidia kuwapa posho wazee wanaoishi katika Mazingira magumu katika  Kata hiyo kila mwisho wa mwezi, kadhalika kuwaongezea  posho  walimu na watumishi wa Zahanati ya Kata hiyo wawe wanafanya kazi kwa bidii .

Hata hivyo amejibu kuhusu kero ya kuchelewa kubebwa taka amesema changamoto iliyopo ni miundombinu ya barabara ambapo magari ya taka yanapokwenda kutupa taka hukaa foleni Dampo kusubiriana kumwaga taka na alilifuatilia hilo suala na wameshakaa na wazabuni hao wamesema wanalifanyia kazi hivyo wananchi wawe wapole .

Pia  kuhusu suala la Mfereji ambao hujaa maji machafu na hawajui chanzo kimeanzia wapi ameshatafuta Mhandisi atakuja naye kufanya uchunguzi wa kina na suala hilo litapatiwa ufumbizi hivyo amewasihi nao waache tabia ya kutupa taka ngumu katika mifereji kwani hupelekea kuziba na maji kukwama kutotembea kwenda Mtoni .

 Sambamba na hayo amejibu kero ya kutozwa tozo wanaopaki magari pembeni. ya nyumba zao kwa kusema wanalifuatilia na Taruara na washaambiwa jukumu hilo litarudi mikononi mwa halmashauri ya Kata na madeni ya nyuma waliyoandikiwa ataomba wafutiwe hivyo wasiwe na wasiwasi.

Diwani Lyoto ameongeza kwa kusema kuwa kipaumbele chake ni elimu kutokana na Vijana wanaohitimu darasa la Saba hawajui kingereza na wanapokwenda kidato cha kwanza hukutana na lugha ngeni hivyo  kuanzia mwakani Shule ya Msingi Mzimuni itakuwa na English Medium kwa wanafunzi wanaonza darasa la kwanza  hivyo hakuna haja ya wazazi kuwepeleka watoto wao katika Shule nyingine.

Diwani Lyoto ameongeza kuwa kutokana na changamoto ya walimu wa Sayansi katika Sekondari za Kata hiyo, amekuwa akitumia Fedha yake kuwalipa posho ya shilingi laki tano kila mwezi walimu wanaojitolea.

Kwa upande wa afya amesema kwamba wakati akishughulikia watu wote wapete bima ya afya, ameeleza ataanza kutoa bima ya afya kwa wazee 100 pia ameahidi pia kufanya maboresho ya Zahanati ya Kata hiyo ili akina mama wasihangaike kwenda Mwananyamala kufuata huduma za afya.


Akizungumzia michezo, ameeleza kuwa atatoa jezi kwa timu zote za Mzimuni, na kuwataka Vijana kufanya mazoezi kwani michezo ni ajira ameahidi kuwapeleka China kwa ajili ya kufanya majaribio kucheza mpira na huko watakaofanya vizuri watabaki kucheza mpira wa  kulipwa.

No comments:

Post a Comment

Pages