Na Magrethy Katengu
Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) latarajiwa kufunguliwa Juni 24 na kilele chake kuwa Julai 2, 2023, huku likikutanisha watanzania na wageni kutoka nchi mbalimbali zaidi ya 200,000 visiwani Unguja litakakofanyika tamasha hilo.
Akizungumngumza jijini Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu wa Tamasha hilo Profesa Martini Mhando alipokuwa akitangaza siku ya ufunguzi wa tamasha amesema kabla ya tamasha hilo wamepokea filamu 3,000 kutoka kila kona ya dunia, huku zilizotoa Afrika Mashariki zikiwa 206 na filamu kutoka Tanzania pekee zikiwa 64.
“Juni 24 ndiyo itakuwa siku ya kufungua tamasha itakuwa ‘Married To Work’, inayohusisha vituko vya wapendanao lakini ikiwa na mambo kadhaa yanayohusuTanzania licha ya kufanywa na mtu kutoka nje.
“Mambo hayo ni kuionyesha Zanzibar kama kisiwa cha ajabu cha mapenzi na ndoto , lakini pia kutakuwa na waigizaji wa Tanzania kimataifa ukiiona utaelewa kwa nini Ziff waliona inafaa kuzindua msimu wa 26 wa tamasha hilo,”amesema Profesa Mhando.
Hata hivyo Profesa Mhando anasema dhamira ya tamasha hilo katika msimu wa 23 ni kuendelea kukuza filamu kimataifa, mawasiliano, haki za binadamu na uhuru kupitia programu mbalimbali zinazofanyika wakati wote linapofanyika.
Amesema kwa kulinda juhudi na mapambano ya uhuru wataonyesha filamu za kumbukumbu za Corridors of Freedom (1990), na Pamberi ne Zimbabwe (1980), zikionyesha mapambano ya ukombozi wa Afrika pia filamu hizo zitaonyesha namna ambavyo Afrika ilisimama kuhakikisha nchi za Afrika zilizokuwa hazijapata uhuru zinaupata
Amesema pia wakati wa tamasha hilo kutakuwa an warsha 12 zitakuwepo zikijumuisha za kurekodi sauti kwenye filamu, huku miongoni mwa watoa elimu baadhi ya warsha hizo ni mshindi wa filamu fupi ya Oscar ‘An Irish Goodbye’, James Martin.
Akizungumzia faida ya waigizaji wa Tanzania kushiriki katika tamasha hilo, mwigizaji mkongwe Ahmed Olotu, maarufu mzee Chillo amesema kuwa kupitia Ziff amekutana na watu wengi wanaowezesha mnyororo wa thamani katika tasnia ya filamu.
Amesema katika tamasha hilo kuna fursa nzuri za kujielimisha ikiwamo uandaaji wa mwongozo wa filamu, uigizaji, utayarishaji sauti, ambazo zinafundishwa na magwiji wa tasnia ya uigizaji.
“Nimejitahid kushiriki katika tamasha hilo mpaka nimeanza kujulikana na filamu ya ufunguzi iitwayo ‘Married To Work’, nikiwa na mwigizaji Idris Sultan, hii filamu imetayarishwa na Mkenya, lakini kutokana na kushiriki katika warsha mbalimbali nimekutana na wakongwe ambao si rahisi kukutana nao kirahisi na wamenitambua na matunda ninayaona,”amesema Chillo.
Akilizungumzia hilo Profesa Mhando amesema kuwa kuna watoa mada katika warsha zitakazofanyika kwenye tamasha hilo, ambao wakisimama mara moja kufundisha kwenye vyuo, matamsha na kwingineko kwa saa moja hulipwa Euro 300. “Hizi siyo fursa za mchezo, waigizaji, watayarishaji, waandishi wa muswada wa filamu na wote waliomo kweye tasnia waitumie nafasi hiyo kujichotea ujuzi.
“Lakini kwa Watanzania mwako wa kushiriki waesha hizi ni mdogo mno, nje ya nchi wanazipenda na mpaka sasa tumepokea maombi 20 ya watu kutoka nje, nawakumbusha wa ndani jiandikisheni kushiriki kwani mwaka huu tutawachukua 17 tu,”amesema Profesa Mhando.
No comments:
Post a Comment