NA STEPHANO MANGO, SONGEA
WENYEVITI wa Mitaa wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt Damas Ndumbaro kwa kitendo chake cha huruma na kuwajali watoto 25 wanaoishi kwenye mazingira hatarishi na wasiokuwa na wazazi kwa kuwasomesha na kuwalipia huduma mbalimbali.
Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti na Wenyeviti hao wakati wakizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Songea Mjini ambayo yametokana na usimamizi wa Mbunge wa Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbaro.
Alon Mhagama ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Mitendewawa alisema kuwa watoto hao wamekuwa wakilipiwa ada, sare, nauli, madaftari na matibabu kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne, jambo hilo ni kubwa sana na Mbunge wetu anapaswa kupongezwa kwa kazi hiyo kubwa.
Mhagama alisema kuwa msaada huo unawasaidia watoto hao kuendelea na masomo ili waweze kufikia ndoto zao ambazo wamejiwekea, hivyo juhudi hizo ambazo anazifanya Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt Ndumbaro zinapaswa ziungwe mkono na kila mdau wa maendeleo.
Naye Yukundus Komba Mwenyekiti wa Mtaa wa Muhumbezi alisema kuwa Mbunge Ndumbaro anaendelea kutekeleza ahadi mbalimbali ambazo ameziahidi kwenye Jimbo hilo ikiwemo la kuwachukua baadhi ya watoto (Wanafunzi) waliohitimu darasa la saba kuwapeleka shule za Sekondari za kulipia kwa gharama za Mbunge huyo.
Komba amesema kuwa Mbunge Dkt Ndumbaro amekuwa akitekeleza ahadi mbalimbali za Jimbo hilo ikiwemo suala la kuwasomesha baadhi ya wanafunzi kwenye shule za Sekondari wakiwemo wanafunzi waliokuwa wakilelewa kwenye baadhi ya vituo vya watoto wenye mazingira hatarishi(YATIMA).
Kwa upande wake Adam Limalikilo ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Mashujaa amesema kuwa Mbunge amefanya jambo kubwa na la mfano mbele ya wakazi wa Jimbo la Songea mjini hivyo amewaomba wazazi kuwasimamia watoto wao ili waweze kufanya vizuri kwenye suala zima la elimu kwa kudhibiti utoro mashuleni.
Kwa upande wake mmoja wa walezi Rosemary Haule kutoka katika kituo cha Swacco amemshukuru mbunge huyo kwa kazi ya kukubali kuwachukua watoto hao na kuwapeleka shule ya Sekondari jambo ambalo amesema linaleta faraja hata kwa walezi wa watoto hao.
Naye wa kituo cha St.Tereza Galus Mpepo amewaomba na wadau wengine waweze kujitokeza kuiga mfano wa mbunge Dkt Damas Ndumbaro kwani watoto hao wanaotokea katika mazingira hatarishi wametoka kwenye moja ya familia ambazo zipo kwenye jamii hivyo wakisaidiwa elimu watakuja kuisaidia tena jamii yetu kwa kufanya kazi mbalimbali.
Akizungumza ofisini kwake katibu wa Mbunge huyo Joel Ndunguru alisema kuwa mpaka sasa Mbunge amefanikiwa kuwasomesha watoto 25 katika shule ya Sekondari ya Daora ya Jijini Dar Es Salaam ambayo ni moja ya shule zinazodaiwa kufanya vizuri hapa Nchini katika suala zima la taaluma.
Ndunguru alisema kuwa Mbunge Dkt Ndumbaro ameendelea kutekeleza ilani ya Uchaguzi katika sekta zote kwa kasi kubwa sana kwa kushirikiana na Baraza la Madiwani, viongozi wa Chama na Serikali na kwa namna ya pekee kabisa anamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini kumteua kushika nafasi ya Uwaziri, pamoja na kulipatia jimbo hilo fedha za kutekeleza miradi ya maendele
No comments:
Post a Comment