HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 14, 2023

MGOGORO WAPANGAJI KARIAKOO KUPEWA NOTISI KUHAMA SIKU 90 WAZUA SINTOFAHAMU


Na Magrethy Katengu


Wapangaji  na Wafanyabiashara wa   Kariakoo zaidi ya 200  wameiangukia serikali kuwasaidia baada ya siku za hivi karibuni Shirika la nyumba la Taifa NHC kuwapatia barua ya notisi kuwataka kuhama ndani ya Magorofa hayo ndani ya siku 90  huku wakiwa hawajui pa kwenda na wakiwa na maduka magodauni yaliyojaa bidhaa ambazo hazijanunuliwa  wakiwa na mikopo ya mabenki hawaelewi hatma yao itakuwaje.


Wakitoa malalamiko kwa  Mwenyekiti wa wakazi hao, Shafiq Mohamedi amesema kuwa ni kweli wameridhia serikali kufanya maboresho ya mji lakini sasa muda waliopewa kuhama ni mchache wengi wana mikopo bidhaa zipo magodauni hatua hiyo imestua walio wengi kubomolewa magorofa zaidi ya 19 kwa mara moja  hivyo wanaiomba kuangalia  hali zao kwani wengine wana mikopo na hawajui watarejeshaje  hivyo wameomba waongezewe muda ili waweze kujipanga na serikali ifanye maboresho ya magorofa hayo Moja moja siyo yote kwa pamoja. 


"Kiukweli majengo yaliyomengi ni chakavu na tunapenda maboresho yafanyike kwa kujengwa upya tusieleweke vibaya  sisi sio kama tunaipinga serikali hapana ila tunachotaka kwanza tusikilizwe lakini pia tupewe muda wa kutosha ili tujue hatma yetu na ubomoaji uanze gorofa Moja baada ya jingine siyo kubomoa yote kwa mara moja siko la kariakoo itapoteza mandhari zuri ya kuvitia kuitwa soko la Kimataifa "amesem7a Mwenyekiti. 


Kwa Upande wake Mpangaji Intehaz Sajan Upanga East Mtaa wa Lugalo Plot no 99 block (11) ametoa malalamiko yale kwa kusema wamekuwa wakiishi hapo na wamekuwa wakichangishwa fedha za maboresho na kusema wao ni watumishi wa NHC pasipokuwa na vitambulisha vya kazi hivyo wamechangizwa pesa nyingi na hakuna kinachoendea .


"Katika magorofa haya sisi wengine ni wamilki tulinunua tangu enzi za babu na bibi zetu na tumeishi na kama wapangaji kutokana na sera na hivyo sasa hii barua tuliyoletewa ya kubomoabomoa hatuelewi tunaomba mtusaidia tusije tukapiteza mitaji yetu" amesema


Naye Prabliyor Kaur amesema suala limeitiza familia yake kwani Kuna mzee anamiaka zaidi mika 32 ni miaka 5 na hawajui na familia yake waende wapi hivyo serikali yetu iliyo chini ya Rais Dkt Samia Hassani ni sikivu itawasaidia


Kwa Upande wake Meneja habari na Uhusiano na Umma Shirika la nyumba NHC Muungano Saguya akijibu malalamiko hayo kwanza amewaomba radhi kutowahusisha katika mchakato wa kubomoa hivyo amewaagiza kuunda kamati ya watu 10 watakaoingia katika kikao cha bodi NHC kujadiliana suala kwa  pamoja na kuwa na azimio moja ambapo kila mmoja ataridhika hivyo amewaomba wawe wapole wasubiri majibu kutoka kamati illiyondwa. 


"Laiti kwamba NHC mngetushirikisha kuhusu uboreshaji wa majengo sisi tusingeshindwa wenyewe kuboresha lakini kinachoonekana hapa ni ujanja ujanja leo unalala unaamka unapewa notice ya siku 90 na notice yenyewe inaletwa siku sita baada ya kutolewa", amesema Msaji.


Amesema ni vyema Rais Samia kutumia busara ya kuona ni namna gani wataweza kuboresha na sio kuwavunjia kwa kipindi kifupi.


"Sisi wafanyabiashara tuna mikopo mbali mbali tunayokopa kwa ajili ya kuzungushia biashara na tuna mizigo kibao sasa unapotupa notice ya siku 90 unategemea sisi marejesho tutarejesha vipi  hela ,"amesema shafiq.

No comments:

Post a Comment

Pages