NA MWANDISHI WETU
NAHODHA wa Yanga Bakari Mwanyeto na kiungo wa kazi Zawadi Mauya wamepongezwa kwa kitendo chao cha kuanzisha taasisi ijulikanayo kama Mwamnyeto Foundation.
Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma "Mwana FA" alipokuwa akizungumza hivi karibuni wakati akienda kuwapa moyo wachezaji wa timu ya taifa waliokuwa kambini wakijiandaa na mechi dhidi Niger.
Mwana FA alisema hakuamini aliposikia kuwa wachezaji wameanzisha taasisi hiyo ni jambo la kupongezwa na la kuungwa mkono na kila atakayeguswa na taasisi hiyo.
Alisema kuwa jambo hilo sio geni kwa wanamichezo wa hapa Tanzania kwani nahodha wa timu ya taifa (Taifa Stars) Mbwana Samatta na mwanamuziki Ally Kiba wana taasisi ijulikanayo kama SAMAKIBA Foundation.
Mwana FA, alibainisha kuwa kitendo hicho walichokifanya kinagusa jamii hivyo uongozi wa Yanga na mashabiki unapaswa kuwaunga mkono nyota hao.
"Yanga ina mashabiki wengi na hivyo kwa kauli moja kama wataamua kuwaunga mkono watafanikiwa kwani hilo ni jambo kubwa katika jamii" alisema Mwana FA.
Naibu waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Muheza mkoani Tanga amewaambia wachezaji hao milango iko wazi kwemda ofsini kumuona kwa ajili ya ushauri namna ya kuweza kufanikisha jambo hilo.
No comments:
Post a Comment