HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 25, 2023

Beki Yanga apewa somo

NA MWANDISHI WETU


BEKI wa zamani wa pembeni aliyewahi kukipiga Yanga na Simba, Amir Maftah amemtaka beki David Brayon aliyekosa namba katika kikosi hicho cha jangwani kujifua wakati wa mapumziko ya ligi.

 


Amir amesema Bryson ni moja ya mabeki bora Tanzania na hakufurahishwa na kupotea kwake uwanjani na sasa ndio muda wa kuwaonyesha watu ubora wake.

 
Akizungumza na Habari Mseto mapema wiki hii alisema anachotakiwa kufanya kwa wakati huu wa mapumziko ni kutafuta kocha maalum ambaye atampangia mazoezi ya kufanya ikiwezekana atafute timu ya mitaani au hata vituo vya kufundisha soka (Academy) kwa ajili ya kujiweka sawa.

 
Mwamba huyo aliyekuwa kipenzi cha timu alizochezea kama Mtibwa, Yanga na Simba ana amini ujio wa kocha mpya katika timu mambo mengi yanaanza upya.

 
"Kocha wa Yanga ameondoka hivyo Yanga lazima watafute kocha mwingine hivyo Bryson ana nafasi ya kumuonyesha mwalimu mpya kuwa ana uwezo mkubwa kwani msimu uliomalizika majeraha yalikuwa yanamuangusha " alisema Maftah.


Aidha  Maftah amebainisha kuwa ikatokea Bryson akaachwa katika dirisha hili la usajili ana amini ana uwezo mkubwa wa kupata timu nyingine ya Ligi Kuu.


No comments:

Post a Comment

Pages