Na John Richard Marwa
Timu
ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'imetanguliza mguu mmoja mbele katika
harakati za kuwania kufuzu Afcon 2023 baada ya kuibuka na ushindi wa bao
(1-0) dhidi ya Niger.
Mchezo huo umemalizika jioni ya leo katika
Dimba la Benjamin Mkapa na Taifa Stars kuibuka na ushindi huo ambao
umeifanya kujiimarisha nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi F
wakifikisha pointi Saba wakisaliwa na mchezo mmoja dhidi ya vinara
Algeria ambao wako dimbani leo kumenyana na Uganda.
Stars ilianza vema mchezo wa leo kwa mashambulizi makali lakini walikosa muunganiko wa kutengeneza nafasi na kuziumia.
Bao la Stars limewekwa kimiani na Simon Msuva akimalizia krosi ya Novatus Dismas na kuipatia Tanzania alama tatu muhimu ambazo zilihitajika kwa udi na uvumba.
Kwa matokeo hayo Stars itahitaji sare ama suluhu dhidi ya Algeria huku wakiiombea Uganda kupoteza mchezo wa leo dhidi ya hao hao Algeria ambapo Stars itafikisha alama nane.
Kama Uganda watapoteza mchezo wa leo dhidi ya Algeria watasaliwa na alama nne na kama wwatashinda mchezo wa mwisho dhidi ya Niger watafikikisha pointi Saba.
No comments:
Post a Comment