HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 18, 2023

𝗠𝗜𝗟𝗧𝗢𝗡 𝗔𝗡𝗨𝗞𝗜𝗔 𝗨𝗡𝗬𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 '𝗧𝗥𝗬 𝗔𝗚𝗔𝗜𝗡' 𝗔𝗧𝗔𝗡𝗚𝗔𝗭𝗔 𝗩𝗜𝗧𝗔 𝗠𝗦𝗜𝗠𝗨 𝗨𝗝𝗔𝗢

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi klabu ya Simba Salim Abdallah 'Try Again' amefichua mikakati ya Simba kuelekea msimu ujao

Baada ya Simba kukosa mataji kwa misimu miwili mfululizo 'Try Again' amesema unyonge huo hautakuwepo msimu ujao, wamejipanha kushinda kila mashindano watakayoshiriki

"Tunaleta wachezaji bora wenye hadhi ya kuichezea klabu ya Simba ambao tunaamini wataweza kutusaidia kutimiza malengo yetu katika mashindano ya ndani na yale ya CAF kwa kuanzia 'Super League' na ligi ya Mabingwa," alisema Try Again

Simba inaendelea kufanya usajili wa maana ambapo inaelezwa kuwa tayari imeonyesha nia ya kumnasa  kiungo Milton Karisa (27) anayekipiga katika klabu ya Vipers Fc ya Uganda

Kiungo huyo ambaye amewahi kufanya kazi na kocha mkuu wa Simba Robertinho Olivieira ikiwa dili lake litajibu atakuwa miongoni mwa nyota watakaokutana na watani zao wa Jadi Yanga kwenye mechi za ushindani

Yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda, 'The Cranes' kinachofanya maandalizi ya mechi za kufuzu Afcon 2023

Nyota huyo bado ana mkataba wa mwaka mmoja na timu yake hivyo mabosi wa Simba wanapiga hesabu za kuvunga mkataba wa kiungo huyo..

No comments:

Post a Comment

Pages